JUA MAPENZI YA MUNGU JUU YA HUYO MTU MAPEMA
Kumpenda mtu sio kigezo pekee cha kumuona huyo mtu kama mke au Mume, Mungu anaweza akaruhusu ukampenda mtu ili tu uweze msaidia aweze vuka mahali fulani katika maisha yake au pia inawezekana Mungu akamleta mtu ili amtumie kukufundisha baadhi ya vitu katika mahusiano vitakavokusaidia katika ndoa. Kwahiyo kabla yakuanza kupiga hatua kubwa tafuta kujua mapenzi ya Mungu juu ya huyo mtu unaempenda au anaekupenda,kujua mapema kutakusaidia kutoumia pindi mahusiano yanapokwisha
KUA HALISI UNAPOKUA NA UNAEMTARAJIA KUWA MUME/MKE
Ni kipindi kizuri kufahamiana tabia halisi za mtu na nihatari kujitahidi kuficha baadhi ya vitu wakati unajua ni tabia yako,ni ukweli kwamba sio kila tabia unaweza kuiacha ni bora mwenzako akajua hiyo tabia na kujipima kama ataweza kuubeba huo udhaifu kuliko ukaficha na kwenye ndoa vikaibuka; kua na uhakika hiyo ndoa itakua kajehanamu kadogo. Nakama ukiamua kubadili tabia unayojua badili kwanza watu unaokua nao mda mrefu na unaozungumza nao ndio mana neno linasema
“Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.” (1 KOR. 15:33)
“Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.” (1 KOR. 15:33)
MSIFANYE MAMBO YA NDOA KABLA NDOA
Uthamani wa Mwanamke huongezeka pindi mwanamme anapokua anamhitaji zaidi ila kila mwanamke anapokua anajirahisisha kwa mwanaume ule uthamani unapungua. Mfano mdada kufanya kazi za kufua, kupika, kudeki, na kulala kwa mwanaume kabla ya ndoa huku hupelekea mwanaume kuona amepata anachokitaka kwa hiyo maranyingi mahusiano haya huvunjika na kushindwa kufikia hatma.Hakuna umuhimu wakufuga kuku kama nyama na mayai yake vinapatikana kirahisi
“Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.” (MIT. 4:19)
“Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.” (MIT. 4:19)
MSHIRIKISHE MWENZIO MAONO YAKO
Maono uliyonayo ndo picha ya maisha unayoiendea, kama ni mwanamke mshirikishe mwenzio mapema ili ajue kama anaweza kuibeba ama hawezi, ni vizuri kufahamishana mipango yenu ya badae mapema kwani kwa kufanya hivo kutamfanya mwenzako apate picha halisi unampango wakuwa nani miaka kumi ijayo.
SAHAU YALIYOKUTOKEA MAHUSIANO YA NYUMA
Watu wengi sana wanaingia kwenye mahusiano mapya wakiwa na majeraha ya mahusiano yaliyopita au wanaingia ili kumkomesha yule alieachana nae huku wakiwa bado na majeraha,kufanya hivo kunapelekea unaingia kwenye mahusiano mapya lakini bado umebeba matatizo ya uhusiano uliopita,kama ulieachana nae alikua sio mwaminifu na unaingia kwenye mahusiano mapya huku ukiwa na majeraha ni rahisi sana ukampigia simu mpenzi wako na asipompokea ukawaza kuwa labda anakusaliti na hiyo itapelekea mahusiano kuvunjika so hakikisha unapona na kusahau yote ya nyuma ndo uingie uhusiano mpya maana ukiingia na majeraha ya nyuma utakua unajilazimisha kufurahi lakini moyoni ni huzuni
“Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo.” (MIT. 14:13)
“Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo.” (MIT. 14:13)
MTAZAMO WAKO UWE KUSULUHISHA NA SIO KUACHANA
Wapenzi wengi wanapogombana utaona wanakimbilia kuachana na hii ni kwasababu kichwani mwao hawana jingine zaidi ya kuachana. Nilazima wapenzi kichwani kuwe kumejaa shauku yakutaka kusuluhisha kila tatizo linapotokea, lazima ifike sehemu ufikirie kama uko kwenye ndoa unafanyaje ? Tabia yakutafuta utatuzi inatakiwa kujengwa tangu mahusiano yakiwa machanga na usizani itajengeka yenyewe ukiwa umeingia kwenye ndoa,tabia huitaji muda kujengwa na huitaji muda kubomolewa. Maamuzi ya kuachana maranyingi huletwa na hasira na neno la Mungu linasema hivi juu ya hasira
“Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.” (MIT. 15:18)
“Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.” (MIT. 15:18)
TUMIA WINGI KWENYE MAHUSIANO NA SIO UMOJA
Hakuna kitu kinafurahisha na kinatia moyo kAma unapomuona mwenzio anazungumzia wakati ujao na anatumia wingi,mfano. Nyumba yetu itakua nzuri,watoto wetu watasoma wapi?,kuliko yule mtu anaesema gari langu,nikijenga nyumba yangu.Kuongea kwa wingi kunaonyesha bado kichani mwako unampango wakuwa nae
EPUKA UONGO KWENYE MAHUSIANO
Wako watu wanapenda sana uongo mpaka wakati mwingine wanaweza kujidanganya wao wenyewe wakikosa wa kumuongopea, kunamtazamo wakidunia kua bila uongo mahusiano hayawezi kwenda mbali si kweli kabisa. Ambapo hakuna ukweli panakosa uhuru maana utajitahidi kuulinda uongo wako miaka yote na kukufanya kukosa uhuru na amani katika mahusiano, nivizuri saana tukawa wakweli kwenye kila kitu tunachokifanya; itatupelekea kuwa huru na kutufikisha kwenye ndoa mana biblia inasema hivi kuhusu uongo; “Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Wala asemaye uongo hataokoka.” (MIT. 19:5)
No comments:
Post a Comment