I. Moja ya hitaji kubwa kabisa katika ndoa ni heshima – hasa kwa wanaume. Waefeso 5;33
Amplified “vivyo hivyo kila mmoja wenu ( pasipo udhuru) ampende mke wake kama vile ni
nafsi yake mwenyewe na mwanamke ahakikishe kuwa anamheshimu na kumpa nafsi yake
mumewe ( kwamba anamtambua, anamheshimu, anampa nafasi stahili, anampa kipaumbele,
anamweka juu ya yote na anampendelea, anamsifu, na kumpenda, anamhamakia zaidi)”
A. Nini maana ya kumheshimu? Kuheshimu, kumhamaki, kumpa thamani.
1. 1Petro 3:1-6Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu, ili kama wako wasioamini lile
Neno, wapate kuvutwa na mwenendo wa wake zao pasipo neno, 2kwa kuuona utakatifu
na uchaji wa Mungu katika maisha yenu. 3Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama
vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. 4Badala
yake kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa ndani, kwa uzuri usioharibika, wa
roho ya upole na utulivu, ambako ni kwa thamani sana machoni pa Mungu. 5Kwa kuwa
hivi ndivyo walivyokuwa wakijipamba wanawake watakatifu wa zamani,
waliomtumaini Mungu. Wao walikuwa ni watiifu kwa waume zao, 6kama Sara
alivyomtii mumewe Abrahamu, akamwita ‘bwana.’ Ninyi ni watoto wa Sara kama
mkitenda yaliyo mema na bila kuogopa jambo lo lote.
2. 1Petro 3:7 Vivyo hivyo ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, nanyi wapeni
heshima mkitambua ya kuwa wao ni wenzi walio dhaifu na kama warithi pamoja nanyi
wa kipawa cha thamani cha uzima, ili kusiwepo na cho chote cha kuzuia maombi yenu.
3. Shetani yuko kazini kumshusha mwenzi wako machoni pako. Matengano na uharibifu.
Kutafuta makosa si kuwa kiroho! Kuwa kiroho ni kuweza kuacha nyuma mabaya yote
na kuangalia yaliyo mazuri.
4. Mwenza ni mzuri, wa thamini alinunuliwa kwa damu ya Yesu!
5. Waone wengine kuwa bora zaidi yako.
a. Wafilipi 2:3-4Msitende roho moja na kusudi moja. jambo lo lote kwa nia ya
kujitukuza, bali kwa unyenyekevu, kila mtu akimhesabu mwingine bora kuliko nafsi
yake. 4Kila mmoja wenu asiangalie mambo yake mwenyewe tu, bali pia
ajishughulishe kwa faida ya wengine.
b. Si sahihi kumbeza mwenzi wako. Kufanya utani na chakula chake, kumdhihaki
anaposhindwa kitu fulani.
B. Kwa maneno – Ongea kwa heshima na mwenzi wako.
1. Hakuna kulaumu – Mithali 14:1 “Mwanamke mwenye hekima huijenganyumba yake,
bali mpumbavu huibomoa nyumba yakekwa mikono yake mwenyewe”
a. Wewe si Roho Mtakatifu kwa hiyo mwache Mungu amshughulikie si wewe!
b. Hakuna mtu anayemtaka mtu ambaye kila wakati anajaribu kuwabadilisha na
haeidhiki na vile walivyo. Tunapaswa kuwakubali vile walivyo kwa wakati huu na
kumwacha Mungu awape ufunuo wa namna ya kuwabadilisha.
c. Mume wako anaposhinda wewe unakuwa mshindi! Mume wako anapopendeza
wewe unapendeza – unaonekana vizuri! Vivyo hivyo na watoto.
2. Sema maneno ya kuwapongeza – sifia mafanikio yao, angalia vitu vya kusifia.
a. Ninapenda mtu anayeweza …
b. Wewe una nguvu, mtanashati, msafi, nk.
C. Tumia muda mzuri naye – Muunganiko usiomeguka katika mahusiano huja kwa kutumia
muda pamoja na mtu huyo. Maana yake kutumia muda mzuri katika mahusiano ya kindani
kufanya vitu vya kuurahisha.
1. Washauri wa ndoa wanasema tutumie masaa 15 ya muda mzuri pamoja na wenza wetu.
2. Mtoe nje mwenzi wako
3. Wengi wakati wanachumbiana wanaumia muda pamoja ndiyo sababu wanataka
kuolewa. Kwanini hamtumia muda tena na kuwa na maongezi ya ujirani sana baada ya
kuoana.
D. Ombeaneni.
1. Kila mara lazima uwe unamwinua mwenzi wako kwa maombi na kuwafunika. Si
kuwabadilisha bali kuomba.
a. Wabadiriki katika kazi zao, kulea watoto na ndoa.
b. Upendo –
i . Mithali 5:15-19,Kunywa maji kutoka kisima chako mwenyewe, maji
yanayotiririka kutoka kisima chako mwenyewe. 16Je, chemchemi zako zifurike
katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani? 17Na viwe vyako
mwenyewe, kamwe visishirikishwe wageni. 18Chemchemi yako na ibarikiwe na
ufurahie mke wa ujana wako. 19Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri, matiti
yake na yakutosheleze siku zote, nawe utekwe daima na upendo wake.
ii . Mithali 31:11,12, Mume wake anamwamini kikamilifuwala hakosi kitu cho
chote cha thamani.12Humtendea mumewe mema, wala si mabaya,siku zote za
maisha yake.
iii . Waefeso 5:22-33, Ninyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana.
23Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Kristo alivyo kichwa cha
Kanisa,ambalo ni mwili wake, naye Kristo ni Mwokozi wake. 24Basi, kama vile
Kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume
zao kwa kila jambo. 25Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo
alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake 26kusudi alifanye takatifu,
kilitakasa kwa kuliosha kwa maji katika Neno lake, 27apate kujiletea Kanisa
tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lo lote, bali takatifu lisilo na hatia.
28Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao
wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29Hakuna mtu
anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama
Kristo anavyolitunza Kanisa Lake. 30Sisi tu viungo vya mwili Wake. 31“Kwa
sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana
na mkewe na hawa wawili watakuwa mwili mmoja.” 32Siri hii ni kubwa, bali
mimi nanena kuhusu Kristo na Kanisa. 33Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende
mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu
mumewe.
iv . 1Wakorintho 13:4-8 Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni
wivu, hauna majivuno. Upendo hauna kiburi. 5Haukosi kuwa na adabu. Upendo
hautafuti mambo yake, haukasiriki upesi, hauweki kumbukumbu ya mabaya.
6Upendo haufurahii mabaya bali hufurahi pamoja na kweli. 7Upendo huvumilia
yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote. 8Upendo haushindwi
kamwe. Lakini ukiwepo unabii, utakoma, zikiwepo lugha zitakoma, yakiwepo
maarifa yatapita. Weka uzio wa ulinzi kuwa zunguka.
c. Waefeso 1:17-22 Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa
utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi.
18Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini
mliloitiwa, utajiri wa urithi wa utukufu Wake kwa watakatifu 19na uweza Wake
mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza huo unaofanya kazi ndani
d. yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno 20ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka
kwa wafu, akamketisha mkono Wake wa kuume katika mbingu, 21juu sana kuliko
falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika
ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia. 22Naye Mungu ameweka vitu vyote
viwe chini ya miguu Yake na amemfanya Yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili
ya Kanisa,
i . omba hii kwa ajili ya mumeo..
E. Weheshimu kwa kuwa jirani kimwili – Moja ya hitaji kubwa la mwanamume katika
kumsaidia kuwa mwenye nguvu katika uana ume wake ni kumheshimu na kumpa mguso wa
jirani kwa kujamihiana. Hii ni moja ya njia mwanamume anajiona ni mwenye mafanikio.
1. Mwanamume anajikabidhi kwako kabisa kuwa mwaminifu hivyo anakuwa hana
uchaguzi mwingine. Lazima utimize hitaji hili kwake.
2. Mara 2-3 kwa siku kama lazima! Ruhusu kisima chake cha upendo kijae.
3. Wanaume wanapaswa kuwa kumbatia wake zao na kuwapenda na SIYO kuwapa
muhadhara kunapokuwa na kosa. Mwanamke hataki kurekebishwa bali msaada wako.
4. Wanawake wanataka wewe pia uonje maumivu yao. Anahitaji kukumbatiwa na kutiwa
moyo wakati anapitia shida. Mwanamke anataka umsikilize na kuongea naye. Anataka
mapenzi unapomkumbatia, mbusu, mpapasa, mbembeleza, kumpa zawadi na kumtumia
ujumbe na kumpigia.
Maswali Ya Majadiliano
• Maeneo gani unaweza kubadilisha kile unachosema na mwenzi wako na watoto wako?
• Mpango gani unaweza kuufanya ili kutumia muda pamoja na mwenzi wako? Nini unaweza
kuondoa katika maisha yako ambacho si cha muhimu ili uweze kuboresha mahusiano katika
mahusiano yako?
• Umewahi kumdharau mwenzi wako au kumlaumu? Unawezaje kuanza kujenga nyumba yako
kwa mikono yako badala ya kuobomoa?
Kuwa Mtendaji Wa Neno
Andika orodha ya vitu unavyotaka au unavyotamani kuhusu mwenzi wako. Anza kuongea maneno ya
kuvithibitisha na kuvitamani kwa vitu vile unavyotamani kwaajili kwake.
Mstari Wa Kukumbuka
Waefeso 5:33 “Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake
mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe. ”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
For booking +255 (0) 744 402 005 MR PEACE PAUL Director| Editor |coral grandig|logo animation|motion graphics
Afya/apostlelucasfredy/comedy/food/marriage/models/Photographer/Relationships/Religious/wedding/suits
No comments:
Post a Comment