Kipanda uso ni ugonjwa gani?
Kipanda uso ni maumivu ya kichwa ambapo kichwa kinagonga kweli kweli na mara nyingine inaweza kuwa sehemu ya mbele au upande mmoja wa kichwa ndiyo unapatwa na maumivu haya.
Maumivu haya yanaweza kubaki kwa saa 4 mpaka saa 72. Vile vile dalili za ugonjwa huu zinatofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine.
Dalili za Kipanda Uso:
Unaweza kupata baadhi ya ishara za ugonjwa huu kama vile;
1. Kujisikia uvivu,
2. Kutapika,
3. Mauzauza,
4. Kusikia kelele sikioni nk.
Wakati mwingine kabla ya kipanda uso watu wengine wanaweza kupatwa na miwasho, shingo nzito, kupiga miayo, kusikia njaa nk
Sababu za kutokea kipanda uso mara nyingi ni pamoja na:
1. Mfadhaiko wa akili (stress)
2. Kelele nyingi kuzidi
3. Kuluka kula mlo
4. Pombe
5. Sigara
6. Shinikizo la chini la damu
7. Kutokunywa maji mengi kila siku
8. Kukosa usingizi
9. Aleji
10. Harufu kali
11. Mkao mbovu
12. Kubadilikabadilika kwa homoni.
Wapo watu haiwezi kupita wiki bila kunywa aina fulani ya dawa kutuliza maumivu ya kichwa au kipanda uso. Hata hivyo matumizi hayo ya mara kwa mara ya hizo dawa mwishowe huleta madhara makubwa katika afya.
Kwahiyo, kwanini sasa usijisomee hapa na ujipatie ufahamu juu ya dawa za asili za kuondoa maumivu ya kipanda uso zisizo na madhara yoyote baadaye?
Endelea kusoma …
Kipanda uso na tiba yake:
Hizi ni dawa mbadala au dawa asili 8 unazoweza kuzitumia unapopatwa na kipanda uso ili kuondoa maumivu hayo na hatimaye kupona kabisa:
Dawa za asili 8 zinazotibu kipanda uso kwa haraka
1. Siki ya tufaa na asali
“Siki ya tufaa ni moja ya dawa za asili zenye viinilishe vingi mhimu kwa afya..”
Pamoja na mengine mengi unaweza kutumia siki ya tufaa kujitibu na matatizo kama kisukari, kutibu kipanda uso, kupunguza maumivu ya mifupa na kuondoa tatizo la kufunga choo. Kwahiyo kwanini usiijaribu siki ya tufaa kutibu kipanda uso chako?
Tumia kwa kufuata maelezo yafuatayo:
a) Weka kijiko kimoja cha siki ya tufaa ndani ya kikombe kimoja cha maji (robo lita)
b) Ongeza asali kijiko kimoja
c) Changanya vizuri
d) Kunywa mara moja mchanganyiko huu kwa siku mara 1 ili kutibu kipanda uso.
Unatakiwa uendelee kutumia dawa hii kwa majuma kadhaa mpaka umepona.
Muda wowote ukipata maumivu ya kipanda uso tena unaweza kuchukua vijiko viwili vya siki ya tufaa na unywe kupunguza hayo maumivu.
2. Kipande cha barafu
Pengine kutumia kipande cha barafu ndiyo dawa rahisi zaidi ya asili ya kutibu kipanda uso. Itakusaidia kupunguza maumivu yatokanayo na kipanda uso. Unapotaka kutumia kipande cha barafu kutibu kipanda uso fuata njia hizi:
a) Tumia kitambaa safi na ufunge kipande cha barafu katika hiki kitambaa
b) Weka barafu ndani ya kitambaa ukipitisha pole pole kwenye paji la uso na shingoni kwa dakika 15 hivi
c) Fanya zoezi hili kila unapotokewa na maumivu ya kipanda uso
3. Pilipili kichaa na limau
Pilipili kichaa ni dawa nzuri ya asili pia kwa kutibu kipanda uso. Inaweza kuongeza wingi na msukumo wa damu mwilini. Vile vile hutumika kutibu hata kuondoa maumivu mengine ya kawaida ya mwili.
Hivyo ikikutokea kipanda uso fuata njia hizi kwa kutumia pilipili kichaa na limau:
a) Chukua nusu kipande cha pilipili kichaa na uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto.
b) Changanya vizuri
c) Ongeza kidogo asali au maji maji ya limau ndani yake
d) Kunywa maji hayo kutwa mara 1 ili kutibu kipanda uso kinapokutokea
4. Chai ya Tangawizi
Tangawizi ni dawa nyingine ya asili ya kutibu kipanda uso. Tangawizi inaondoa uchovu, inasaidia kuweka sawa homoni, husaidia kutanuka kwa misuli na kuondoa maambukizi kwenye mishipa ya damu.
Kwahiyo mara upatwapo na kipanda uso jaribu kufuata njia ifuatayo ukitumia tangawizi kujitibu kipanda uso:
a) Tengeneza chai ukitumia tangawizi freshi (mbichi) na unywe kikombe kimoja mara 2 au 3 hivi kwa siku. Usiweke majani ya chai humu.
b) Au wakati mwingine maumivu ya kipanda uso yakikujia chukua kipande cha tangawizi mbichi na utafune. Itakuondolea hayo maumivu na uchovu pia.
5. Mafuta ya ufuta na unga wa mdalasini
Unapopatwa na kipanda uso au hata maumivu ya kawaida ya kichwa dawa nzuri kabisa ni kufanya masaji ya kichwa. Kufanya masaji ya kichwa kutasaidia kutibu kipanda uso sababu masaji inaziba ishara za maumivu zinazotumwa kwenda kwenye ubongo.
Masaji pia inaongeza ufanisi wa kazi wa homoni iitwayo ‘serotonin’ ambayo inahusika na kuweka utulivu wa akili na kukupa usingizi. Kwahiyo utakapopata kipanda uso tena fanya yafuatayo:
a) Chukua vijiko vikubwa viwili vya mafuta ya ufuta na uyapashe kidogo katika moto
b) Changanya na nusu kijiko kidogo cha unga wa mdalasini na nusu kijiko kidogo kingine cha iliki ya unga ndani ya mafuta ya ufuta
c) Pakaa mchanganyiko huu kwenye paji lako la uso
d) Jimasaji pole pole
e) Acha hivyo kwa lisaa limoja hivi
f) Jisafishe na maji ya uvuguvugu
Fanya zoezi hili kutwa mara 1 kila siku mpaka umepona
6. Tufaa (Apple)
“Tunda moja la tufaa kwa siku linatosha kuondoa uhitaji wa daktari.”
Kula matunda ni afya au ni jambo zuri kwa afya yako. Matunda ya tufaa (au epo) ni matunda yenye viinilishe mhimu sana kwa ajili ya mwili kiasi kwamba ukiwa na tabia ya kula tunda hili moja tu kwa siku hutakuwa na hitaji lolote la kuonana na daktari.
Tufaa ni tunda maarufu sana duniani na lina faida nyingi zinazoweza kutumika kutibu maradhi mengi. Mara tu unapopatwa na maumivu ya kipanda uso kwanini usijaribu kula tufaa? Unachotakiwa kufanya ni kula tu hili tunda mara tu unapopatwa na maumivu ya kipanda uso.
Kitendo hiki cha kula tu hili tunda kitakuondolea hayo maumivu na baadhi ya tafiti zinasema ukinusa tu ganda la kijani la tufaa inasaidia pia kupunguza maumivu ya kipanda uso.
7. Kahawa na Limau
Kahawa ina kaffeina ambayo inaweza kuziba baadhi ya vipokezi na mishipa ya damu kutuma ishara au ujumbe wa maumivu katika ubongo. Kwahiyo kikombe kimoja cha kahawa kinaweza kukusaidia kuondoa maumivu ya kipanda uso.
Kwahiyo wakati utakapopata kipanda uso kunywa kikombe cha kahawa na ukihitaji matokeo mazuri zaidi basi ongeza kijiko kidogo kimoja ndani yake cha maji maji ya limau.
Mhimu tafadhali: Pamoja na kuwa kahawa inaweza kutumika kwa ajili hii kama dawa ya kutuliza kipanda uso bado nakuonya usizidishe matumizi ya kahawa kwani kaffeina iliyomo kwenye kahawa ina madhara mengine mabaya kiafya ukizidisha kuitumia.
Hivyo kipanda uso chaweza kuongezeka zaidi kama utazidisha kunywa kahawa.
8. Chumvi
Chumvi pia ni dawa nzuri ya kutibu kipanda uso. Kama unataka kutumia chumvi kutibu kipanda uso fanya hatua zifuatazo:
a) Andaa maji ya kuoga ya moto
b) Weka chumvi kikombe kimoja au viwili (chumvi ya mawe ndiyo nzuri zaidi)
c) Tumbukiza mwili wako wote ndani ya haya maji kwa dakika 15 hivi na utulie.
d) Hii itakuondolea au kuzuia maumivu wakati ukipatwa na kipanda uso.
Maumivu yakizidi muone daktari.
kinanisumbua sana kipanda uso ahsante kws elimu hii
ReplyDeleteNaombeni ushaur juu kipanda uso kinansumbua
ReplyDeleteJamani Hii tatizo inasumbua familia yangu
ReplyDeleteKinaniuma Sana hiki kipanda uso naombeni msaada Hadi sasa nipo kitandani naumwa
ReplyDeleteNaishi kyela mwenye uwezo wa kunipatia dawa ya kipanda uso please tuwasiliane 0753009566
ReplyDelete