Namna Kansa inavyojitokeza mwilini
Siku hizi tunaambiwa mtu mmoja kati ya watu watatu atakuwa na mojawapo ya aina za kansa, miaka 65 iliyopita ilikuwa mtu mmoja kati ya watu elfu kumi.
Kansa ni nini?
Kansa ni mgawanyiko usio sawa na usiodhibitika wa seli na kuunda uvimbe unaovamia na kuzidhuru tishu.
Seli za kansa husambaa kupitia mikondo ya damu au kupitia vungu (cavities) mbalimbali za mwili na kuunda uvimbe wa pili katika sehemu nyingine za mwili. Kansa inaweza kushambulia karibu katika kila tishu yeyote ya mwili.
Bado hakuna uhakika wa moja kwa moja wa nini kinachosababisha kansa ingawa inajulikana wazi kuwa, kuwa karibu na baadhi ya vitu (kemikali) kunaweza pelekea kansa.
Tuna seli za ngozi, seli za Ini, seli za ubongo, seli za mapafu, seli za misuli, seli za mifupa na kadharika. Seli hizi tofauti zinatujia toka kwa kinasaba (DNA) chetu ambacho kinamiliki maagizo (blue print) juu ya aina gani ya seli itengenezwe.
Wakati baadhi ya vitu (kemikali) vimechukuliwa ndani ya mwili kupitia ngozi au hewa tunayopumua au kwa njia ya chakula, miili yetu inaweza kuvihimili vingi ya hivyo vitu kabla ya safari ya mwisho kuingia kwenye vinasaba vyetu na kusababisha seli zisizo za kawaida kutengenezwa na kupelekea kile tunachokiita KANSA.
Miili yetu lazima iachwe katika hali ya ualikalini kidogo na siyo katika asidi kabisa isipokuwa kwa kipindi cha muda mfupi, kinyume chake madhara lazima yatatokea kwenye tishu, ogani, seli na mwisho kwenye kinasaba ambako seli hutengenezwa.
Kuna namna tatu ambazo zimebuniwa ili kuishughurikia asidi: mfumo wa mkojo, mapafu na tumbo.
Mfumo wetu wa mkojo hupitisha asidi nje ya mwili. mapafu yetu huchukua ndani oksijeni na kutoa nje gesi ya kabonidayoksaidi (co2) ambayo ni asidi. Hii ndiyo njia namba moja miili yetu iwezavyo kuitoa asidi ambayo ni taka za seli.
Tumboni mwetu ndimo haidrokloriki asidi hutengenezwa na kuhifadhiwa ikisubiri kutumika wakati chakula kinaliwa. Haidrokloriki asidi hii inahitajika na mwili ili kuuwezesha mwili kuyatumia madini yanayopatikana kwenye vyakula tulavyo.
Baada ya hii haidrokloriki asidi kuwa imeandaliwa (opened up the food), valvu ya chini ya tumbo itajifungua na chakula huenda ndani mwanzoni mwa utumbo mdogo ambako asidi hupunguzwa makali (neutralized) na bikaboneti toka katika kongosho.
Ikiwa asidi hii haikurekebishwa vya kutosha na baadhi ya asidi inaingia katika utumbo mdogo, asidi hiyo itaziathiri seli za tishu na kwa kipindi cha muda mrefu itaathiri kinasaba na unapata kuzarisha seli zisizo za kawaida na kupelekea kansa ya utumbo mdogo (intestinal cancer).
Wakati asidi hii inaingia kwenye mkondo wa damu ikitokea kwenye utumbo mdogo hupelekwa kwenye ini ambako damu husafishwa na asidi hurekebishwa.
Ini letu haliwezi kuhimili kiasi kingi cha asidi inapotokea tunakunywa kiasi kingi cha vinywaji vyenye kabonidayoksaidi (the carbonation), ni kiasi kidogo kinachopatikana katika soda, bia na shampanye (champagne).
Ubongo wetu unatambua damu hiyo yenye asidi nyingi lazima irekebishwe kwa haraka, hivyo utaamuru kalsiamu itolewe toka katika mifupa yetu ili kuirekebisha damu hiyo. Ukopaji huu wa kalsiamu kutoka katika mifupa kama hautalipwa kwa wakati, utapelekea matatizo mengine ya kiafya kama vile ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).
Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH (potential hydrogen). Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.
Unaweza kukinunua kipimo cha PH na kupima Ph ya mate na mkojo, hii itakupa mwelekeo wa namna gani unafanya kuitunza 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako.
Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.
Haidrojeni ina chaji chanya (+), wakati alkalini ina chaji
hasi (-). Kila mtu anapaswa kula zaidi vyakula vyenye alkalini (matunda na mboga za majani) na kunywa vinywaji vyenye asidi chache, alkalini nyingi kama juisi ya limau, ya chungwa, ya zabibu na maji halisi.
Maeneo ndani ya mwili ambayo hayana mtiririko wa moja kwa moja wa damu yanaweza kupatwa na asidi kwa urahisi zaidi.Tishu zitaisajiri asidi hiyo na kihisio maalumu (special sensor) ambacho kitapeleka ujumbe kwenye ubongo kama MAUMIVU.
Kunakokuwa na damu chache au hakuna mtiririko wa moja kwa moja wa damu kama vile kwenye maungio, katileji na uti wa mgongo, maeneo haya yanaweza kupungukiwa kwa urahisi madini, chumvi, maji na elektrolaiti na kusababisha misuli iliyo karibu nayo kufanya kazi zaidi ya uwezo wake na kusababisha uwezekano wa kukakamaa kwa mishipa, madhara kwenye misuli na kwenye mafundo (ligaments).
Maumivu ambayo hayakusababishwa na jeraha au ajari, ni kiashiria kuwa tishu, ogani, maungio na seli vina asidi iliyozidi ambayo inahitaji kufanywa alkalini.
Kwa kunywa glasi moja (ml 250) ya maji halisi na kuchukua kipande cha chumvi ya baharini, kutapunguza kama siyo kuondoa kabisa maumivu. Jaribu hii kwa kunywa glasi moja ya maji na kisha kuiweka chumvi mwishoni mwa ulimi wako na kuiacha iyeyuke kwa dakika na kisha isafishe kwenda chini na glasi ya pili ya maji. Kwa mjibu wa dr.Batman, kitendo hiki kitabadili PH ya damu, tishu, ogani na seli ndani ya mwili.
Asilimia 94 ya damu ni maji, ubongo wetu una zaidi ya asilimia 85 za maji, na tishu zetu laini zina asilimia 75 ya maji.Tunatumia maji kupumua nje, kila masaa 24 tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumua tu nje.
Chukua kioo, hemea juu ya kioo, utaona ukungu (maji).
Kumbuka kuwa hali hiyo ya uasidi wa tishu, ogani, na seli, mwisho itaingia kwenye kinasaba (DNA) chetu na kubadili mpangilio (codes) na kusababisha seli mbovu kutengenezwa ambazo tunaziita ‘kansa’.
Kansa inaweza kuishi katika mazingira ya uasidi na uanaerobiki, yaani katika upungufu wa oksijeni pekee.
Ikiwa kinga yako ya mwili inafanya kazi vizuri, itakuwa na seli nyeupe za damu ambazo zinaweza kutengeneza oksijeni na kuitoa ‘haidrojeni peroksaidi’ kama inavyohitajiwa kuzuia kutengenezwa kwa seli za kansa.
Dr.Batman anafafanua katika vitabu vyake kuwa, wakati mtu anapokuwa katika upungufu wa maji na chumvi (out of balance in cells), mwili utajifunguwa na kuizarisha histamini ili kujiwezesha kuiweka upya seli katika usawa wake, kupiga chafya ni angalizo kuwa histamini imeamushwa.
Moja kati ya madhara ya histamini ni kuisimamisha seli nyeupe ambayo hutengeneza haidrojeni peroksaidi kwenye mfumo wetu wa kinga ya mwili.
Kwa sababu ya biashara kuunda vyakula vyetu vyote maalumu na vinywaji vyenye radha mpya, radha nzuri na nguvu ya kutosha kwa kutumia kafeina toka katika mimea na mitishamba kama vile ginseng kuisisimua tezi ya adreno, kunasababisha Ini kutoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa.
Hakuna nguvu iliyomo kwenye kafeina au ginseng. kuna majina mengine mengi ya visisimuaji hivi kama vile, kokwa za guru, kokwa za cola na mfalme wa yote ni guarana. Mbegu za guarana zina kiasi cha kafeina mara tatu zaidi ya zile za kahawa, na hawatakiwi kuliorodhesha neno kafeina kwenye vifungashio (packages) au kontena.
Ungaunga wa guarana hutumika kutengeneza vidonge vya kupunguza uzito kwa sababu kafeina itazisambaratisha hisia za njaa, lakini hakuna mahala neno kafeina linaonekana kwenye kifungashio.
Kuna mimea, kokwa na kemikali nyingi ambazo zitaisisimua tezi ya adreno na kusababisha ini kuitoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa au hata kuitengeneza toka tishu za mwili wenyewe.
Kafeina kama kikojoshi, huyalazimisha maji kukimbia nje ya mwili kwa haraka na kuziacha seli bila muda wa kutosha kuyatumia maji hayo, maji yanapokimbia kwa haraka nje ya mwili huyakimbiza pia madini mhimu nje ya miili yetu.
Nguvu safi katika mwili wa binadamu huja kutoka katika maji/chumvi na potasiamu ambavyo huwasha pampu za majenereta machache yaitwayo kwa kitaalamu ‘cation pumps’, umeme wake huifadhiwa katika beteri ziitwazo “Adenosine Triphosphate”(ATP) na “Guanosine Triphosphate”(GTP).
Aina nyingine ya nguvu kwa mwili inatokana na sukari. Inahitajika sukari zaidi kuzarisha kiasi sawa cha nguvu izarishwayo kwa maji/chumvi na potasiamu, ni kama vile umeme wa maji (haidroelectric power) dhidi ya umeme uzarishwao kwa makaa ya mawe.
Wakati sukari inapochomwa kuzarisha nguvu, huzarisha taka nyingi zaidi (oxidation) zinazohitaji vidhibiti zaidi vya taka hizo (anti-oxidants) ili kuirekebisha hali hiyo ya taka za sumu. Ikiwa mtu hali matunda na mboga za majani vya kutosha, basi Ini lazima lizitumie asidi amino zenye umhimu sana kama vidhibiti vya taka hizo.
Tunapokula vyakula vya asidi vilivyoongezwa utamu kama kemikali na kemikali vihifadhio, jumlisha vinywaji ambavyo ni asidi na vimeongezwa utamu kama kemikali; vitakuwa vikiuandaa mwili kupata ‘kansa’.
Moja ya sababu kuu ya mtu kutakiwa kula matunda na mbogamboga ni kuwa vyakula hivi ni alkalini, wakati nyama, kuku, samaki, nyama ya nguruwe, pasta na mayai ni asidi.
Wengi wetu siku hizi tunakula vyakula ambavyo vimekwisha andaliwa (fast food) na hatutumii vyakula vyenye alkalini ya kutosha. Kumbuka kuwa kabonidayoksaidi ni asidi pia kama ilivyo kwa kahawa, chai na alikoholi ambavyo huathiri PH ya damu na tishu.
Madawa na wewe, kwa mjibu wa dr.Earl mindell, mwandishi wa kitabu; ‘Earl mindell’s new vitamin bible’ (zaidi ya nakala milioni 10), anasema katika ukurasa wa 414 wa kitabu hicho kuwa ‘kafeina ni dawa yenye nguvu kubwa, uwezekano ni kuwa, hauifurahii tu kahawa au cola yako ya kila siku, bali umekuwa mtegemezi (addicted) kwavyo’.
Kafeina inafanya kazi moja kwa moja kwenye mfumo mkuu wa fahamu (central nervous system). Inakupa hisia safi kwa haraka na kupunguza uchovu. Inasisimuwa pia kutolewa kwa sukari iliyokuwa imehifadhiwa kwenye Ini ambayo inatumika kama kiinuzi (lift) kwa kahawa, cola na chokoleti (The caffeine big three), lakini faida hizi zinaweza kuzidiwa uzito na hasara zake.
Utolewaji wa sukari iliyokuwa imehifadhiwa, kunapelekea mfadhaiko mkubwa kwenye mfumo wa dharura wa mwili. Unaposhitushwa kidogo tu, unakuwa na nguvu za haraka kushughurika na tatizo. Hali hii hatimaye inawezapelekea kukauka kwa tezi ya adreno kutakakosababisha damu chache yenye sukari (hypoglycemia), udhaifu, na kuumwa sana iwapo sukari haitachukuliwa mapema kupandisha juu damu sukari.
Pia dalili za uchovu sugu zinaweza kujitokeza kwa sababu mwili utakuwa umelazimishwa kutengeneza sukari toka katika tishu, mishipa na umbile lake wenyewe, kitendo hiki huitwa kwa kitaalamu kama ‘Gluco-neogenesis’, yaani kutengenezwa upya kwa sukari toka katika hifadhi ya mwili na kisha toka katika tishu, mishipa na umbile lake wenyewe (mwili).
Imethibitika pia kuwa kafeina imekuwa ikiingilia na kuathiri unakilishaji wa kinasaba (DNA), namna ambavyo seli mpya hutengenezwa. Kafeina inaweza kusababisha upotevu toka mwilini wa vitamini nyingi za kundi B, kundi C, zinki, potasiamu na madini mengine. kahawa huongeza hali ya uasidi kwenye utumbo mdogo. Kafeina inaweza kusababisha msukosuko ndani ya mwili.
Kafeina siyo kwamba tu huimaliza nguvu iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ubongo, bali pia huzuia mfumo vimeng’enya katika kutengeneza kumbukumbu kwenye ubongo.
Jarida moja la afya la Uingereza, ‘The British Medical Journal Lancet’, limeripoti uhusiano mkubwa uliopo baina ya utumiaji wa kahawa na kansa ya kibofu cha mkojo na kupungua kwa uzarishaji wa mkojo.
Kituo cha sayansi kwa masirahi ya umma (Center for science in public interest) kimewashauri kinamama wajawazito kukaa mbali na kafeina kwa kuwa tafiti zimeonesha kwamba kiasi cha kafeina kilichomo kwenye vikombe 4 vya kahawa kwa siku kinaweza kusababisha matatizo wakati wa kujifungua kama yalivyoonwa katika majaribio kwa wanyama.
Dr.Batman anafafanuwa pia kuwa, kunywa maji kunahitaji kiasi cha chumvi kuchukuliwa pia ili kuzirekebisha taka (haidrojeni) kutokana na maji kutotumika kwenye seli. Haidrojeni ni asidi.
Damu yetu ina chumvi na kongosho letu lazima liwe na chumvi ili kuitumia kutengeneza bikaboneti inayotumika kurekebisha asidi ndani ya tumbo.
Siku hizi vyakula vyetu vingi vinazarishwa kwa kutumia mbolea kemikali na kupuliziwa tena kemikali ili kudhibiti wadudu waharibifu. Tunatumia kemikali kali kwenye vyakula vyetu ili kuvihifadhi kwa matumizi ya baadaye. Miili yetu lazima ishughurike na kemikali hizi kila siku.
Siku hizi, kemikali zinazotumika kuongeza utamu kwenye vyakula zinasababisha matatizo makubwa kwenye miili yetu kwa sababu zina radha ya utamu lakini hazina sukari.
Sukari ni asidi, lakini kemikali zinazotumika badala ya sukari zinasababisha madhara zaidi ya sukari halisi kwa mjibu wa dr.Batman na madaktari wengine wengi duniani.
Baadhi ya kemikali hizi kali zipatikanazo kwenye vyakula vyetu nyakati hizi zinabaki na kujishikiza kwenye utumbo mdogo na kuendelea kurundikana na hivyo kuufanya utumbo usifanye kazi zake vema.
Ini letu pia litazishikilia baadhi ya kemikali hizi kali ambazo zinaingia kwenye damu na kujaribu kuzirekebisha kadiri liwezavyo. Ini litaendelea kuzihifadhi kemikali nyingi kadiri liwezavyo mpaka litakaposhindwa na kuamua kuzitupa tena kwenye mkondo wa damu na kwenda kwenye kila seli mwilini.
Kwa sababu hii, ndiyo maana watu wengi siku hizi wanatumia dawa rafiki na vifaa maalumu kusafisha utumbo mdogo na Ini kila mara ili kuziondoa taka hizi na uzito zinaouongeza tumboni. Kisha mtu analazimika kuwa mwangarifu sana kuepuka vyakula ambavyo vina kemikali kali nyingi.
Damu yote hupita kwenye Ini na amino asidi zinatumika kuzirekebisha sumu (poisons) ambazo huliingia Ini. Wakati Ini linapokuwa katika upungufu wa amino asidi hizi, litalazimika kukopa baadhi toka katika ogani zingine kama vile Kongosho. Kitendo cha kongosho kukopwa amino asidi zake kutapelekea matatizo mengine kwenye kongosho kama vile kisukari, na uwezekano wa kutokea kwa kansa ya kongosho (pancreatic cancer) ikiwa amino asidi zilizokopwa hazikurudishwa kwa wakati ili kuliwezesha kongosho kuendelea na kazi zake vizuri.
Miili yetu ilisanifiwa kula vyakula halisi vya asili (fresh natural grown food) au kula nyama iliyouliwa wakati huo huo (fresh live kill).
Kwa njia za kijenetiki, siku hizi tumebadili vyakula vyetu ili kupata mavuno mengi. Tunawalisha wanyama wetu vitu (kemikali) ili kuwafanya wakue haraka na kuongezeka uzito kwa haraka. Tumekuwa wafugaji wa samaki pia ili kukidhi mahitaji na kuepukana na bei kubwa zitokanazo na gharama za kutumia meli za uvuvi na matatizo ya hali ya hewa.
Siku hizi sote tunaharaka katika kila jambo, hatuna muda wa kutosha, kitu kinachotusababishia wengi wetu kutokula mlo kamili wenye matunda halisi na mboga za majani.
Masaa 24 kwa siku seli zinaunguza kaboni kama mafuta (cells burning carbon) ili kutuacha katika hali joto ya nyuzi joto 37.5. Unapochoma kitu chochote, kinatoa nje taka moshi. Taka zote hizo toka katika seli zote za mwili, lazima zirekebishwe kwa muda wa masaa yote 24 kwa msaada wa matunda na mboga za majani.
Asidi amino zina umhimu mkubwa kwa afya bora. Ubongo wetu lazima upate kusambaziwa asidi amino kila siku ili ufanye kazi. Ini haliwezi kufanya kazi vizuri bila uwepo wa asidi amino. Mishipa yetu lazima iwe na amino asidi, kila seli kwenye mwili wa binadamu inazihitaji amino asidi au asidi ambazo zimetengenezwa toka asidi amino ndani ya mwili.
Deoxyribonucleic acid (DNA), Ribonucleic acid (RNA) na Decosahexaenoic acid (DHA), zote ni asidi.
Tunapopumua katika hewa iliyochafuliwa kama vile moshi wa magari, miili yetu lazima izitumie asidi amino hizi kuirekebisha sumu hiyo kadiri iwezekanavyo.
Gari huyaunguza mafuta ya kaboni kwa kutumia oksijeni na kutoa nje taka (moshi) ziitwazo ‘kabonimonoksaidi’. Moto wa kuni pia huzarisha moshi. Hata uchomaji wa mafuta safi huzarisha taka ziitwazo kabonimonoksaidi.
Kwa hiyo mtu anapoamua kuvuta sigara, anakuwa ameamua kuvuta ndani kabonimonoksaidi ambayo ni sumu kwa mwili wa binadamu. Uvutaji wa sigara pia unasababisha upungufu wa oksijeni mwilini, hii inamaanisha kuwa baadhi ya seli ndani ya mwili hazipati oksijeni ya kutosha na zinapatwa na asidi toka katika kabonimonoksaidi. kitendo hiki kitapelekea siku moja kutokea kwa kansa katika sehemu dhaifu za mwili.
Watu wengine hawajawahi kuvuta sigara lakini wamepatwa na kansa ya mapafu. Kila mwili wa mtu lazima ukope asidi amino na hivyo kupunguza usambazwaji mzuri wa oksijeni kwenye baadhi ya sehemu za mwili ili kukutetea uendelee, kwa matumaini kuwa utaupa mwili unachokihitaji siku za mbeleni ili kuyarudishia maeneo yaliyokopwa amino asidi zake.
Unajiuliza kwanini watu wanavuta? wote wanajibu kuwa wanaifurahia. Unaenda kufa kwa sababu fulani kwa namna fulani. kuvuta kunawafanya wajisikie vema.
Wakati mtu anajaribu kuvuta kwa mara ya kwanza, mapafu yake hujifunga na atakohoa kwakuwa mapafu yanajaribu kuitoa kwa haraka hewa iliyochafuliwa (moshi). Lakini atakapojaribu ‘puff’ ya pili, mwili wake utaitoa kemikali iitwayo ‘endorphinsi’ ili kumuwezesha kuhimili (kuvumilia maumivu) moshi huo mpaka atakapopata hewa safi kupumua.
Ni kemikali hii ambayo mwili unaitoa ndiyo inayomfanya mtu kuwa mtegemezi (addicted) wa kuvuta. kutolewa huku kwa endorphinsi kunamfanya mtu kujisikia ‘super’. Ungependa kuacha sigara na unashindwa? Niandikie nikujibu kwanini unashindwa na ufanye nini utimize azma yako.
Endorphinsi hutolewa pia wakati mama anajifungua kwa sababu ya maumivu. Kwa kawaida ni ngumu sana kwa mwanamke kuacha kuvuta kuliko kwa mwanaume kwa sababu wanawake wana kiasi kingi cha endorphinsi kuliko wanaume.
Unywaji pombe pia unaweza kupelekea baadhi ya miili kuitoa endorphinsi na kumpelekea mtu huyo kuwa mtegemezi wa alikoholi.
Moshi unaweza kunukia vizuri, lakini kamwe hauwezi kuwa mzuri kwa afya zetu. Vinukizi vingi (air fresheners) vinatumia kemikali kali ambazo si nzuri kwetu, baadhi ya mishumaa pia ina kemikali hizo.
Mtu anapaswa kuwa makini na kusoma maelekezo ya kwenye vidandiko vya bidhaa ili kujua ni nini anakula, kunywa, kunusa au anaongeza kwenye ngozi yake.
Inashauriwa pia kuepuka kubaki katika mkao mmoja kwa muda mrefu iwe ni kukaa au kusimama. Watu wengi kutokana na kazi wanazofanya wanalazimika kubaki wamekaa au kusimama tu kwa masaa mengi kwa siku jambo ambalo ni hatari kwa afya kwa kuwa asidi hujikusanya hivyo kwa urahisi zaidi. Yapo mazoezi maalumu ya kufanya kila mara kwa watu wa kazi za aina hiyo ili kurudishia damu katika mfumo na hivyo kutoa nje taka za asidi.
Dr.Batmanghelidj ana shuhuda nyingi kwenye vitabu vyake za watu waliokuwa na kansa zilizofikia tamati. Walipoacha kunywa vinywaji vyenye kafeina na kula chokoleti; na kisha kunywa maji nusu ya uzito wao katika aunsi na kuchukua robotatu gramu za chumvi kwa kila aunsi 16 (ml 500) za maji na kuongeza matunda na mboga za majani zaidi kwenye milo yao na kufanya mazoezi, kansa zao zilifikia kikomo na miili yao kujiripea yenyewe.
Hakuna kansa tena!.
No comments:
Post a Comment