Mwanasaikolojia Chris Mauki azungumza ndani ya Nchi Ya Ahadi jinsi tofauti za kijinsia zinavyoweza kuathiri mahusiano yetu.
Inawezekana sana mwanaume kwa jinsi alivyoumbwa akakupenda siku ya kwanza kwa mengi yale yaliyo nje yako, yeye anajua nini kimemvutia kwako na taratibu mkikubaliana kupendana ndio anaanza kugundua na kuvumbua vilivyofichwa ndani yako na hivyo ndivyo vinamfanya aidha kukukimbia au kugandana na wewe.
Lakini ni vema sana wanaume kujua kuwa siku ya kwanza mwanamke anakuona anavutiwa zaidi na “qualities” zilizoko ndani yako, sio sana vile vilivyoko nje yako. Kwahiyo ongeza juhudi katika kujenga vilivyo ndani yako kwasababu vinamashiko sana katika mahusiano yako kuliko kupoteza muda kujenga vilivyo nje yako wakati havina tija. Ni sawasawa na kutumia nguvu ngingi kutengeneza mtego wa kunasa nguruwe pori huku ukiwa na nia ya kwenda kutega kware.
Siku zote dhana ya mahusiano inaweza kuwa na namna mbili tofauti kutokana na tofauti za jinsia zetu wenyewe. Lakini kwanza tujiulize nini maana ya MAHUSIANO?Mahusiano_ Ni ujenzi wa uhusiano wa kijinsia kati ya mwanaume na mwanamke unaohusisha sana hisia.
TUNAWEZA KUYAGAWANYA MAHUSIANO KATIKA MAKUNDI MANNE.
1> Kundi la watu walio katika mahusiano ya urafiki hadi uchumba.
2> Kundi la watu wanaoanza kujiunga/kujiingiza kwenye mahusiano.
3> Kundi la watu ambao tayari wako kwenye ndoa.
4> Kundi la watu ambao hawajajiingiza kwenye mahusiano kabisa.
TOFAUTI ZA KIJINSIA.
Mara nyingi kunaweza kuwa na tofauti mbalimbali kutokana na utofauti wa kijinsia unaotokana na chanzo au vyanzo mbalimbali vinavyoleta tofauti ambayo inatokana na Asili Yetu.
Asili yetu ni pale mmoja asemapo ''mimi ni mwanaume, yeye ni mwanamke''
VYANZO VYA TOFAUTI HIZI.
a) Malezi.
Mara nyingi malezi ndiyo yanayoweza kuonyesha tabia asilia ambayo anayo mtu kulingana na jinsia yake. Wazazi ndio nyenzo kuu ya kumfanikisha mtoto kuwa na malezi bora yenye mtazamo mzuri wa kuwa na mahusiano mazuri kwa wazazi wenyewe na hata kwa jamii inayomzunguka.
Lazima wazazi watumie vyema fursa zao kuwajenga watoto wao katika misingi iliyo thabiti katika maisha yao yote.
b) Makuzi.
Katika hatua ya ukuaji mzazi ndiye amtengenezaye mtoto katika hatua zote za ukuaji wa kimwili na kiroho kutokana na umri wake.
Utafiti alioufanya Chris Mauki.
Katika utafiti wangu ( Chris Mauki), 2012 huko Afrika Ya Kusini imeonyesha kuwa familia nyingi huwa na mzazi mmoja (single parent family) ambapo watoto huwa chini ya uangalizi wa malezi ya mzazi mmoja, hivyo mtoto huathiriwa kisaikolojia zaidi.
Mfumo/aina za familia:
Familia ni mkusanyiko wa watu wenye uhusiano mmoja na kukaa pamoja.
Aina za familia.
-familia yenye mzazi mmoja na watoto (single parent family)
-familia yenye wazazi wawili (nuclear family)
-familia yenye wazazi, watoto na ndugu wengine (extended family)
-familia ambayo haina wazazi (non-parents family)
c) Watu wanaokuzunguka (marafiki).
Huenda marafiki au watu wanaokuzunguka ndio wanaoweza kuwa chanzo cha kuibua utofauti, kwani unaweza kusikia maneno yanayosemwa kwa kujadili mambo ambayo ni sumu kali ya kuibua tatizo katika jamii.
d) Maisha yako ya awali (life background).
Ujionavyo nafsini mwako ndivyo ulivyo na ndivyo watu watakavyokuona. Maisha yako ya awali yanaweza kukupa swali la kujiuliza; 'jinsi ujionavyo nafsini mwako ndiyo chimbuko la kuibua furaha au huzuni maishani mwako'.
Matatizo ya kimahusiano:
Matatizo siku zote hutokana na namna mtu anavyoweza kujitengenezea mwenyewe.
Lakini matatizo ya kimahusiano watu wengi hushindwa kuyatatua kwa sababu ya kutokujua tofauti zao za kijinsia.
Mifano ya tofauti za kijinsia.
i> Wanawake wengi wameathiriwa na manunuzi (shopping) wakati wanaume hawazingatii sana manunuzi/shopping.
ii> Wanawake wengi hawazingatii sana mpangilio wa muda katika mipango yao. Lakini wanaume wengi huzingatia muda zaidi.
iii> Kwa matumizi ya pesa wanawake hutumia vibaya kuliko wanaume.
Nini tufanye kutatua tatizo?
- Lazima kila mtu aelewe chanzo cha tatizo na kulitatua
- Utayari wa kuchukuliana udhaifu
- Kuendana tabia.
JE! WANAWAKE WANASEMA NINI KWA WANAUME?
Kwa tafiti zilizofanywa nchini, imeonekana kuwa wanaume hawawezi kuelezea hisia zao walizo nazo kwa undani zaidi.
Wanaume pia hawana ukweli katika kuonyesha uhusiano zaidi.
Wanaume wengi wana fikra hasi kwa wanawake.
No comments:
Post a Comment