"Baada ya muda, mapenzi hubadilika na huwezi kuzuia mabadiliko ndani ya mapenzi, maana mabadiliko ni sehemu ya maisha na hio haimaanishi mapenzi ndo yanaisha - MrPeacePaul
"Baada ya muda, mapenzi hubadilika na huwezi kuzuia mabadiliko ndani ya mapenzi, maana mabadiliko ni sehemu ya maisha na hio haimaanishi mapenzi  ndo yanaisha

"Baada ya muda, mapenzi hubadilika na huwezi kuzuia mabadiliko ndani ya mapenzi, maana mabadiliko ni sehemu ya maisha na hio haimaanishi mapenzi ndo yanaisha

Share This
"Baada ya muda, mapenzi hubadilika na huwezi kuzuia mabadiliko ndani ya mapenzi, maana mabadiliko ni sehemu ya maisha na hio haimaanishi mapenzi 
ndo yanaisha!".



  • Rudisha mazingira yaliokuwepo kipindi cha mwanzo mwa mahusiano...
    Baada ya muda kupita tukavizoea vitu na kuviona vya kawaida, binadamu kama ilivyo haja huwa tunapenda kupuuza mambo, tunakua wavivu na kuviondoa vitu vidigo vidogo vilivyokua vinaupa sapotiuhusiano

    , yale mambo tuliokua tunafanya wakati uhusiano bado mchanga inakua hamna tena, zile kadi ya siku ya kuzaliwa tulizokua tunanunua tukiambatanisha na uwa rozi inakua hamna tena, zile hamasa zilizokua zinaletwa na siku ya wapenda nao tunazipuuzia, wakati vitu vidogo vidogo kama hivyo ndo vilikua vinaleta nakshi na changamoto ya kuishikilia nguzo ya mahusiano ikae katika hali ya furaha na kutamaniana kila wakati, cha kwanza kabisa inabidi urudishe mazingira ya mahusiano katika hali iliokuwepo kipindi cha mwanzo.
      • Jaribu kutumia muda pamoja...
      Baada ya kila mtu kuwa na vyake vya kufanya na kuanza kupuuziana, inatakiwa sasa muondoe tofauti na jambo la kwanza mrudishe ukaribu na kuanza kutumia mda pamoja!, mnaweza kufanya shughuri tofauti tofauti ambazo zinaweza kuwarudisha pamoja na kurudisha ukaribu mliokua nao awali. Zile hisia ya kwamba yupo tu haendi popote ndo zinazoingiza uhusiano kwenye matatizo, inatakiwa uupe uhusiano asilimia nzima na kama mkipanga kutumia muda pamoja, msipuunzie mkahairisha kisa kesho ipo!.
      • Mawasiliano ni daraja la mahusiano...
      Hakuna suruhisho wala ukaribu unaoweza kutokea bila mawasiliano toka pande zote mbili, baada ya ugomvi kadhaa, kutunziana visasi moyoni na kulalamikiana kila mtu anavutia upande wake, suruhisho linalofuata ni kuanza kuongea, na kila mtu anatakia abadilike na kukubali sehemu aliokosea, ongea na kusikiliza, sio kuongea tu wewe ndo wewe bila kusikiliza upande wa pili!, ondoa tofauti na ongea kirafiki, baada hapo mnatakiwa kudumisha maongezi hii itawafanya muwe karibu na kuongeza hisia na hamasa ndani ya mapenzi.
      • Muonyeshe unavyomjari...
      Aksante ni neno dogo ila lina nguvu katika mahusiano na inamfanya mtu kujua anajari ulichofanyiwa, rudisha hamasa kwa kumfanyia jambo zuri la kumshtukiza mwenzio kumwonyesha unamjali na bado pendo lako kwake haliwezi isha, ua na kadi yenye neno ''Nakupenda'' linaweza kufanya mapinduzi makubwa sana kwenye uhusiano wa muda mrefu, kama nilivyosema awali mambo madogo madogo ndio yanayobeba hisia nzima na muhimili wa mahusiano!.
      • Rudisha urafiki....
      Mwanzo wa mahusiano kitu kilichokua kinawafanya muwe pamoja ni urafiki, urafiki ndo ulikua unafanya mwende mjini pamoja na kuleta ukaribu na kujaliana, mnaweza kunza kufanya huo urafiki ambao utawafanya mue karibu kwa kuangalia muvi pamoja na kuanzisha mazungumzo endelevu kama ulivyokua unafanya mwanzo wa mahusiano.
      • Fanyeni pati...
      Baada ya kukaa pamoja kwa mda mrefu na ule uwepo wa maboreko ya mda mrefu wa nyie kukaa pamoja unaosababisha kukosa hata kitu cha kuongea, pati inawaleta marafiki wenu karibu na kuwafanya muwe karibu bila haja ya kuongea na inasaidia kuondoa maboreko ya kukosa maneno ya kuongea na kurudisha furaha iliyo potea  kwa kuwaweka mazingira machangamfuu na mkusanyiko wa watu wengi, na pia itatoa wasaha mzuri wa kuchangamsha hisia na hamasa kwenye mahusiano yenu.
      • Tokeni out sehemu ya mbali....
      Kutoka out sehemu ya mbali au kusafiri kabisa inawafanya kuwabadilisha akili kwa kuwaweka mazingira tofauti na yale mliyoyazoea na kuwatengenezea chachu ya kuanzisha mahusiano mapya katika mazingira mapya, hii itawafanya kupata vitu vipya vyakuongelea na kuwachangamsha kitu kinachoweza kurudisha hisia zilizopotea ndani ya uhusiano.
      • Mguso...
      Mguso ni sehemu muhimu ya mahusiano, mguso hua unatengeneza hamasa yake na kutengeneza khali ya kuamini na huleta hisia. Mguso unasababisha mchanganyiko wa kikemikali mwilini ambao hutengeneza msisimko, hali ya kukaa mbali na mwenzio si nzuri, kaeni karibu na kutengeneza mguso ambao utaleta hisia za kuwa karibu na mwenza wako.
      • Muonyeshe uzuri alionao bado upo...
      Onyesha bado yupo moyoni na mwonyeshe jinsi bado anavyokuvutiwa nae, maneno madogo madogo yananguvu yake usiyapuuzie ukaacha kuyasema pale yanapoitajiwa kuyasema, hamna mwanamke anaechoshwa kuambiwa anapendwa, monyeshe unavyompenda kwa jinsi unavyomfanyia mambo madogo madogo ya kila siku, kuwa mbunifu na mshangaze kwa mambo ambayo hatarajii kutika kwako na utaona mabadiliko yanavyorudi na kuongeza hisia kwenye uhusiano wako.
      • Ongeeni juu ya ufanyaji wenu wa mapenzi, vipendezesho na vichukizo...
      Mabadiliko ya ndani yanaanza kwa maongezi ya kuambiana na kujulishana mambo mbalimbali kuhusu ufanyaji wenu wa mapenzi, ambianeni nani anapenda nini na kipi kifanyike kuongeza hamasa katika kuongeza nakshi ya ufanyaji wa mapenzi.
      • Badilisha Mazingira mnayofanyia mapenzi....
      Mabadiliko ya sehemu ambayo mnafanya mapenzi ni nzuri kutengeneza hamasa, hata kama ni sehemu ileile, jaribu kubadilisha hata rangi ya chumba au mkao wa kitanda, uzuri wa mapenzi ni jinsi akili ya mtu ilivyo kwa wakati huo, kwa hio uzuri na mabadiliko ya mazingira yanaweza kusaidia kuweka akili katika hali ya upya na pia jitahidi mabadiliko ya staili, sio kila siku staili ni ile ile nayo inaweza kusababisha maboreko kwa sababu ya mazoea!. 
                    Kama mjomba wangu anavyoniambia ''MABADILIKO HUANZA NA WEWE'' , kama ulikua mbishi, jaribu kubadili mambo unavyofikili, badilisha mtazamo na uwe na mtazamo chanya, kuwa mbunifu wa kufanya michezo midogo midogo, fanya mchezo kwa kubashili kwa uzuri, mpe kitu mpenzi wako kabla hajakiomba uonyeshe jinsi unavyomjua na kumpenda, hamsha hamasa ndani ya uhusiano wa muda mrefu kwa kuzingatia mambo yalio orodheshwa hapo juu.

      No comments:

      Post a Comment

      Pages