Najua uko busy. Wote tuko hivyo. Kuna bills za kulipia mahali kwingi, Kutazama watoto, Kuwapigia watu wa mauzo, kufanya order mbalimbali, kujibu emails, kutatua matatizo.
Kuna mambo mengi sana yanaendelea kwako. Unawezaje kupata muda wa kuchart na marafiki, na hata wale wa nje ya nchi yako, Kupata kikombe cha chai na hata kumkumbatia mtu?
Niamini mimi. ninaelewa. busy ni jina la game. Daima tunafanya, tunatakiwa kuendelea mbele, Daima kujaza masaa yetu , bado tumekwama.Jamii inatuambia nenda, nenda ,nenda, vinginevyo utabaki nyuma. Lakini kusema kweli, Ukiangalia list yako ya siku utaona bado hufanyi vizuri. Unaweza kwenda na kufanya na kumaliza hicho kitu. lakini mwisho wa siku unajikuta hujisikii kama umekamilisha kitu. huwi mkamilifu.
Mpaka hapo Utakapoanza kuuthaminisha muda wako.
Muda wako, Siku yako inathaminishwa na kukamilishwa na maneno ambayo wewe mwenyewe utayatamka Kuanzia asubuhi kabla hujatoka kwenda kwenye kazi zako za kila siku.Ni lazima ukumbuke kusema Bwana ndiye Mchungaji wangu hutapungukiwa na vitu ambavyo unaenda kufanya, na hali ambayo unataka uwe nayo siku nzima, muda wote. Ili siku yako iende kwa utaratibu semea siku yako , Muda wako maneno ya kumiliki .
Siku yako , Muda wako utakuwa na thamani pale utakapoanza kumwambia mtu fulani kuwa unampenda. Utakapoanza kumfundisha mtu kitu cha kumsaidia katika maisha yake, Utakapoanza kupata muda wa kufikiri, Kupata muda wa kupumua kabla ya kuanza kitu chochote. Utakapoanza kuwapongeza watu bila ya kutarajia asante kutoka kwao. Pale utakapoamua kuwepo sehemu ambayo utamshangaza mtu ambaye hakutegemea uwepo wakati huo. Utakapoamua kuongea na kumsikiliza mtu badala ya kutuma ujumbe. Kufanya wema mahali ambapo hutegemei kukubalika.
Siku ambayo utaanza kuwa Rais wa muda wako mwenyewe. Masaa yote 24 yajae kwako.
THaminisha umakini wako, Weka Upendo pasipo na maisha ya upendo.
Fanya muda wako uwe na maana kwa kuongea maneno mazuri ili Mungu akubariki. Chunga maneno yako. Unaweza kuanza meditation kila siku asubuhi kabla ya kwenda popote. Tamka maneno mazuri ya Mungu, tumia Muda vizuri. Pigia wazazi wako simu . mtumie ujumbe mzuri mtu unayempenda
Kuwa mtu wa shukurani kila siku unapoamka. Msikilize mtu bila ya kuangalia simu yako. mtu anapokuhitaji uwepo mahali hapo. Na kila wakati fikiri utatoa nini badala ya kufikiri utapata nini.
Katika maisha ni vizuri kufahamu ni kitu gani unataka. Muda unapita haraka sana usipokuwa makini, Usipokuwa mtu wa kupanga mambo ya kufanya, huna malengo, huna sheria, mipango. Fahamu kitu cha kufanya kila siku.
Wakati mwingine ukitaka kuwa mtu mwema unatakiwa kuvunja sheria. Tunza muda wako . Tafuta taarifa kila siku na uzifanyie kazi. Thaminisha muda wako na maisha yako ya baadae yatakushukuru wewe.
No comments:
Post a Comment