Kuwa na mahusiano mazuri ,badala ya yale mabaya , sio tu kuteka mafanikio bali ni kuwa na mtazamo ulio mzuri kimaisha. Wanandoa ambao mahusiano yao mara nyingi huonekana kukua na kuimarika katika muunganiko wao ,huangalia sana vitu ambavyo vina mtazamo chanya,mtazamo wa maendeleo,hapa kuna aina saba au tabia saba za za wanandoa wanaokuwa na mtazamo chanya unaowafanya wapate furaha siku zote.ni nama gani basi wewe kama wewe kuanza kuwa na mtazamo mpya.
1,WENYEWE HUONA KUWA MALUMBANO YAO HUZAA MJADALA:
Malumbano siku zote kwa wengine huleta ugomvi , lakini wao huona kati ya malumbano yao mengi ni mafunzo. wanandoa waonaona na wanaojua kuwa malumbano huzaa mjadala ,wana mtazamo chanya.kitu zao kinachofanyika huweka mezani tofauti zao na kuchukua muda wa kukaa na kuchangia hisia zao na kuongea ba ya kuhitilafiana , na huepukana na kuita au kuleta wengine katika malumbano yao, na mwisho wa malumbano hupata suluhisho ambalo kwa pamoja huona kama fursa ya wao kuwa na urahisi wa kuepuka kulaumiana.
2.HAWADHURIKI NA HISTORIA HASI ZA MAHUSIANO .
Ukiwa unachunguza vyombo vya habari vinavyoonesha mahusiano mbalimbali yenye furaha na namna ya mahusiano na katika kujadiliana mambo ,au jinsi gani marafiki hujadili mahusiano pindi panapotokea kuhitilafiana inaweza kuharibu uhusiano wenu,maana kila ndoa ina staili yake ya kujadili. maana kuna wengine .
kama wewe sio jasiri katika maeneo hayo,utatetereka,lakini wanandoa walio imara huona na kusikia hizi historia lakini haziwadhuru wala kuingilia katika mahusiano yao pekee na hisia zao, unapoona au kusikia vitu ambavyo sio vizuri vinavyoleta mgawanyiko kuhusu mahusiano, unatakiwa kuwa na msimamo ambao una maamuzi yako hi ni mwenyewe, usibadili msimamo , haijalishi ni nini kinatokea katika mahusiano mengine.
3,KILA MMOJA ANAKUWA HURU:
Kuna wanandoa wengi hufikiri kumbana mwenzi wake ni njia sahihi ya kufanya awe mwaminifu katika ndoa , Sio kweli,! wapo wengine huvizia hata simu za wenzi wao ili kujua kinachoendelea, huo sio utaratibu mzuri, tena si ustaarabu.Wanandoa wenye furaha mara zote hupeana uhuru kwa kila jambo ., lazima utambue kuwa uhuru unapo mpa utamfanya awe mwoga ,tena hatafanya kitu kinyume na mahusiano yenu, hapo ndipo uaminifu utadumuna kuwa na furaha.
4.MARA NYINGI HUTAFANTA NJIA ZA KUFANYA ILI KUWA BORA KATIKA MAHUSIANO YAO:
Unaweza kutafuta njia bora wakati wote katika mahusiano ,wanandoa wanaoona mbali huangalia ubora wa urafiki wao,hujifunza mambo mengi mbalimbali mazuri yanayohusiana na mahusiano ,mara nyingi hupenda kusikiliza historia nzuri zinazotia moyo kujenga , kuna vitu vingi unaweza kujifunza jinsi ya kuwa bora katika mahusiano na pia unatakiwa kuweka juhudi kubwa unapokuwa na mwezi wako ili kuwa bora.
5,HUFANYA VITU VINAVYOTAKIWA KUFANYIKA HATA KAMA SIO WAJIBU WAO
Wanandoa wengi huwa na malumbano juu ya vitu ambavyo vinatakiwa kufanyika huenda ni vya ndani au vya nje, kwa mfano:kufua, kupika na usafi wa nyumba. wana ndoa wenye mafanikio hushirikiana katika vitu muhimu vyote hatakama sio wajibu wao kuvifanya, la ya kusababisha majibishano na malumbano ya kuto kufanya vitu vya nyumbani , unatakiwa ufanye tu wewe mwenyewe na mwenzi wako atafurahia.
6.KILA MOJA HUFURAHIA UWEPO WA MWENZAKE:
Najua kuna wanandoa wengi hupenda kufurahia kutumia mwingi wakiwa na marafiki zao sehemu za starehe au sehemu nyingine , badala ya kutumia muda huona nwenzi wao kwa pamoja.wanandoa wenye furaha huwa hawajali kupoteza muda mwingi na wenzi wao kuliko wanapokuwa na rafiki zao.kila mmoja hufurahia uwepo wa mwe nzake na kila dakika wanapokuwa pamoja
il kuwa katika mahusiano mazuri lazima wote muwe katika ukurasa mmoja katika katika masuala ya, unapenda nini, unataka nini ,unahitaji nini. fanya hivyo ili kuimarisha mahusiano.
7.HUCHUKULIANA,HUBEBEANA MATATIZO KWA PAMOJA:
Watu hujaribu kutatua matatizo peke yao bila ya wenzi wao,lakini wanandoa wanatakiwa kuambiana matatizo kwa sababu unapomwambia wako mtatatua ndani kwa ndani badala ya kutafuta ushauri kwa wengine ,unapokuwa na tatizo usisite kumwambia ili mwenzi wako ili kutaka msaada kwake, maana huyo mtu yupo kwa ajili yako.na ndio atakaekusaidia kwa kadri awezavyo
kuwa na mwenzi inakusaidia wewe wakati ukiwa na tatizo au shida yoyote, maana ndiye mtu ambae mnachukuliana mambo yenu yote .pia itakufanya wewe kuwa mwenzi bora,na kuwa na furaha.
kupitia hizi njia mbalimbali naamini zinaweza kukusaidia kuwa bora nakujenga mahusiano mazuri na mwenzi wako, jaribu leo na utaona itakuaje kwako.
No comments:
Post a Comment