USHAURI WA MAHUSIANO.
Jinsi gani utakabiliana na wivu wa mapenzi kabla wadudu wabaya hawajaanza kutafuna mahusiano yako na umpendae katika maisha yako
Watu wengi husema kuwa mapenzi ni upofu, lakini sio mapenzi yanayoleta upofu bali ni Wivu ndio uletao upofu.
Wivu wa kupitiliza huharibu mahusiano, mpe uhuru mwenzi wako , usipende kumfungia na kumfuatilia kwa sababu ya wivu, mwache aongee na watu , afanye kazi , kwani hata yeye anaelewa kuwa ana mke ampendae au mume ampendae, kwa hio ni ni kitu ambacho kinamfanya awe tofauti na wengine ambao bado hawana wenzi wao.
Ni muhimu kujua tabia zetu na kuzifahamu tabia za wenzi wetu ili kuishi vizuri bila kuwekeana wivu, wivu unaharibu mahusiano hata kama yalikuwa mazuri namna gani.
NINI MAANA YA WIVU KWENYE MAPENZI.
Kiini au mzizi wa wivu ni mtu kuangukia kwenye woga wa kupoteza mpenzi wake, kupoteza heshima uliokuwa nayo, pia woga huo hupelekea kutojiamini ndani ya mahusiano, kuwa na hisia tofauti.
Woga unapotokea wivu huja na zaidi sana unakuwa na hofu , hasiri na chuki ya mapenzi, wakati mwingine kukosa tumaini katika huo uhusiano. hata hivyo endapo mmoja wenu atakuwa na tabia ya kutokujali hisia za mwenzake ,hicho kitu ni kibaya , ni muhimu kujua na kujali hisia za kila upande.
kuna wenzi wengine sio waaminifu hata kidogo , lakini hapa hatuna kithibitisho cha kujua hasa kuwa sio mwaminifu , mara nyingi huwa ni kukisia tu , hasa unapoona kuwa ana wasiliana na watu mbalimbali, na mikutano mingi ambayo huielewi , hapo ndipo panapozaliwa wivu.
lakini hapa tunaangalia vipengele vifuatavyo vya kusaidia kukabiliana na mzunguko huu wa wivu wa mapenzi kwa kuacha kuwapelekesha wenzi wetu na baadae kuchanganyikiwa wenyewe.
1.UWE NA MSIMAMO.
Acha kuhamaki , tawala hisia zako na moyo wako ,jisemeshe mwenyewe kuwa hutaki kuwa na wivu, wivu ndio nini. cha kufanya inabidi kuelewa mazingira ya mwenzi wako , mazingira ya kazi, biashara, elewa ndugu zake , elewa marafiki zake , elewa tabia yake, elewa hisia zake kwako, itakusaidia wewe kutokuwa na wivu. usikubali wivu uje ndani ya moyo wako.
2.JIPENDE MWENYEWE KWANZA.
Kama hujikubali na kujipenda mwenyewe itakuwa ngumu kuwapenda wengine na kuwakubali, watu walio makini na watulivu hawaruhusu hali ya wivu iwavamie, maana wanaelewa madhara yake. kwa hio ni muhimu kujitambua na kujifahamu , tumia muda wako kujitambua sawasawa, tumia uelewa wako na akili zako jinsi ya kukabiliana na maisha ya mahusiano.
3.ACHA KUJIFANANISHA.
Ikiwa unajifananisha utatengeneza mbegu ya wivu inayozaa matunda ambayo utafanya mambo yasiokuwa na akili, kwa sababu utaanza kufuatilia mwenzi wako pasipo sababu yeyote kwa kuwa tu umeona fulani anamfuatilia mwenzi wake.jiamini usiwe mtu wa kuigiza mahusiano, ya kwako ni yako sio ya mwingine.
4.TAFUTA KINACHOKUFANYA UOGOPE.
Je, ni woga wa kupoteza mpenzi ? au hauko makini , au unaona kama hukustahili kumpata huyo ulienae?au labda wewe una tabia hizo , sasa wasiwasi unapata kuwa huenda nae yuko kama wewe? maana ukiwa mwizi utakuwa mwoga sana kila mtu utamwona mwizi kumbe sio.
5.ANDIKA.
Andika kila unachoona kuwa kinakuogopesha ili visiharibu mahusiano yenu, itakuwa ni rahisi kushughulikia tatizo kama utakuwa unaandika yote unayoona yanakusumbua akili, utapata nafasi ya kujitambua, anza kujiuliza kwa nini unasikia wivu?,kwanini hali hii inakuja kwangu, andika kila kinachokuja akilini mwako, na baadae anza kushughulikia moja baada ya lingine. juhudi yako ndio mafanikio yako.
6.UWE MKWELI. JIULIZE..
Hivi kweli hivi vitu vinanifanya mimi nogope kiasi hiki? vitanisaidia nini endapo nitavifuatilia na kupata maumivu ya moyo wangu. kwani nikifuatilia nitakuwa na furaha? sitaki Wivu.
7.TAFUTA NGUVU.
Uwe na mtazamo wako na sifa ya kipekee, uwe mtu wa kushukuru kwa zawadi na baraka ambayo umepata kutoka kwa mungu , kupata huyo mume au mke ulienae.
8. BADILISHA MSIMAMO.
Ukiwa unawaza mabaya tofauti na mazuri itakuwa ni vigumu kufikiria mazuri hata kidogo, utakuwa na mitazaamo ambayo haina matunda mazuri,badilisha tabia na misimamo ya mawazo mabaya ili uwe mtu wa tofauti, ukitulia utaona mambo yakwenda vizuri bila wasiwasi.
9.HIKI NDICHO KITU TUKITAKACHO.
Kwa kuwa tunahitaji kuwaza mazuri, kila mmoja hisia zetu zitapona, na jinsi tunavyoendelea na tabia hii tutajenga mahusiano yenye nguvu. kumbuja kuwa kila upandacho ndicho utakachovuna.
hebu tujaribu kuchukua nafasi au kuvaa kiatu cha mwingine , hali hii ingekukuta wewe ungefanyaje? kaa katika nafasi ya mtu ambaye tayari yuko kwenye wivu kama utaweza.
Basi ukiona watu wamefanikiwa kwenye mahusiano yao furahia, na unaweza kutumia mfano wao katika mahusiano yako ikiwezekana.Upendo ndio kitu kikubwa katika maisha ya kila mwanadamu.
Je wewe unaweza kuepukana na wivu? changia uzoefu wako ili kusaidia wengine.
No comments:
Post a Comment