LOVE NI NINI? - MrPeacePaul
LOVE NI NINI?

LOVE NI NINI?

Share This

Upendo umetokana na neno la kigiriki “ahab aheb” lenye maana hisia kali na muhathirika wa ndani. Upendo ni hisia kali, upendo chimbuko lake ni moyoni upendo ni Mungu ameuweka ndani ya moyo wa mwanadamu, upendo ni maisha ya mtu na ni utaratibu wa mtu hivyo mtu anapo amua kumpenda mtu mwingine mtu huyu anakua ameamua kuhatarisha maisha yake kwa mtu Fulani. Ameamua kuuweka moyo wake kwa mtu Fulani. Ameathirika ndani ya moyo wake kwa ajili ya mtu Fulani akili ambayo ndio chanzo cha mapenzi imekubaliana nayo. Najua kuwa unajua kuwa mapenzi ni akili,kama akili ikichoka hakuna mapenzi hivyo ndio maana hata maandiko yanasema “ Ishini na wake zenu kwa akili”
Maana mapenzi la kweli yanahitaji akili timamu uwe na muda wa kufikiri kabla ujafanya lolote. Kuishi na mtu kunahitaji akili timamu, sasa mtu huyu amefanya maamuzi ya kiakili, kimwili na kiroho kuwa wewe unamfaa hivyo unatakiwa kuyaheshimu na kuyadhamini mawazo yake na kuyatendea kazi kwa uangalifu sana UPENDO NI MSUKUMO WA NDANI YA MTU.
Upendo si kitu cha kuchezea mpendwa mwenzangu. Upendo ni uhai wa mtu. Ndiyo maana maandiko yanasema: “Upendo una nguvu kuliko mauti”
Hili andiko wewe unalielewaje? Mimi ninavyolielewa ni kuwa Upendo ni zaidi ya kifo yaani Upendo ni heri kuchagua kifo kuliko kuchagua kupenda au kupendwa maana upendo umekamata moyo na wewe unaelewa kazi ya moyo kwa mtu? HEART – kwa kiyunani ni (leb) – mind ni ufahamu, midst (labab) Kiyunani – inner person – yenye maana ya undani wa mtu – mind and heart – which also includes decision making ability- (ufahamu na moyo ambayo hujumuishwa pia maamuzi yanaweza kufanyika (Mwanzo 6:5-6) vilevile moyo unasimama kama (kiungo cha mwili) 2Sam 18:14- can be used of the innerman- undani wa mtu unaweza kutumika hivyo.
Moyo unakuwa kama – hisia (emotions Kumb 6:5) moyo – furaha waamuzi 16:25
Moyo una hofu na huzuni ISam 24:10
Moyo unaweza kujaribiwa zab 86:11
Moyo unaweza ukawa mgumu wakati mwngine kumb 30:6
Hivyo maumivu ya moyo sio mchezo, haya ni maumivu ya ndani kwa ndani. Maumivu yake yanatembea ndani ya damu haya ni mateso makubwa sana maana unaweza ukawa umelala mwili lakini nafsi hailali inahangaika usiku kucha – unauwezo mkubwa wa kwenda kulaa umechaka na kuamka umechoka maana nafsi ilikuwa inatafuta.
a) kufarijiwa kutiwa moyo,
b) upendo kudhaminiwa,
c) kuheshimiwa,
d) kukubalika,
e) kutambulika na mtu anayefaa maana upendo hautafuti watu bali unatafuta mtu haijalishi awe amesoma, hajasoma, tajiri au masikini, mweupe au mweusi, mfupi ama mrefu Upendo unamtafuta mtu (a person)
Moyo – ndio eneo ambalo maamuzi yenye nguvu yanafanyika – kuaminiana ndio maana hata maandiko Matakatifu yanasema “Mtu moyoni huamini na kwa kinywa hukiri na kupata wokovu” na andiko lingine linasema
“Watu hawa wananiheshimu kwa midomo tu lakini mioyoni mwao wako mbali nami”
Hivyo upendo wa kweli huanzia moyoni. Unaamini tokea moyoni kuwa huyu ndiyo, anayenifaa katika moyo wangu, unamdhamisha tokea moyoni mwako anakuwa na kibari kikubwa maishani mwako kuwa huyu ndiye kisha kwa kinywa unamdhibitisha kuwa ndiye.
PENZI LA KWELI LINAONGEA MOYONI.
1. Moyo huthibitisha kuwa huyu ndio anayenifaa maishani mwangu.
2. Aliyepata kibali moyoni mwangu.
3. Ndiye niliyemtafuta usiku na mchana.
4. Aliyeutesa moyo wangu.
5. Aliyeuyumbisha moyo wangu mara tu nilipomwaona.
6. Mwenye uwezo wa kutimiliza ndoto yangu.
7. Kioo cha maisha yangu.
8. Faraja wa moyo wangu.
9. Huyu ndiyo mwandani wangu (msiri)
10. Kitambulisho cha maisha yangu.
11. Mbeba maono yangu.
12. Heshima yangu katika jamii itakayo nizunguka.
13. Mtetezi wangu asiyeweza kuvumilia nisipate aibu katika jamii.
14. Mfuta machozi na majasho yangu.
15. Mratibu wa moyo wangu.
16. Chemichemi ya furaha yangu.
17. Barafu wa moyo wangu.
18. Asali wa moyo wangu.
19. Malkia na Mfalme wa moyo wangu.
20. Chanzo cha afya yangu.
21. Mjenzi wa familia yangu.
22. Mwalimu wa familia yangu.
23. Mlinzi wa ndoto na maono yangu.
24. Adui wa adui zangu.
25. Mponyaji wa majeraha yangu yaani doctor wa moyo wangu.
26. Rafiki wa moyo wangu.
27. Ngao ya moyo wangu.
28. Ufunguo wa maisha yangu.
29. Ua la moyo wangu.
Huyu ndiye mpenzi anayetafutwa na mtu yoyote katika Dunia hii ya leo mwenye sifa hizi mpendwa, mapenzi yana nguvu sana kuliko unavyodhania kuna watu walikosea katika kuchagua leo wanalia usiku na mchana ndoa imekuwa ndoano mapenzi yamevamiwa na shubiri, moto umewaka matusi, dharau, kiburi, jeuri, ngumi ndio yamechukua maisha kweli mapenzi yanatesa moyo, yanaumiza, yana katisha tamaa, yana poteza maana ya mtu, yanavuta mauti ukiyakosea utanielewa ninamaanisha nini? –MOYO ndio chanzo cha furaha – ukichafuliwa furaha hukimbia na amani, hapo ndipo hofu inapochukua nafasi unajikuta unaanza kumuogopa mpenzi wako, na wakati upendo wa kweli hauna hofu hata kama mke au mume ni mkali namna gani Upendo wa kweli huondoa hofu lakini ukiona mtu anamuogopa mwenzi wake hapo tambuakuwa penzi hilo limevamiwa na adui, moyo umepoteza dira umekosa matumaini na huyo uliyenaye, Hofu huvuta dhambi hapo ndipo unapoweza kuona mtu anatafuta rafiki mwingine ili aweze kumlinda kumrudishia amani yake, kumponya majeraha yake hapo sio mchezo inabidi unapotambua hivyo unatakiwa kutengeneza maana hapo ndio chanzo cha magonjwa, talaka n.k fanya kwa bidii kujiaminisha katika moyo wa mwenzi wako ili mambo yasiharibike
 Moyo ukiumizwa HUZUNI hutokea hapo ndipo maombolezo yanapoanza, mtu huyu utamkuta analia kila unapomuona na machozi yanamdondoka,
[a] moyo wake unalia.
[b] Moyo wake unatoa damu kidonda kibichi.
[c] Maombolezoyaliyo beba majuto kwa nini nilikubali kuwa na huyu?
[d] Kama ningelijua nisingekubali.
[e] Alitokea wapi huyu, Ee Mungu mbona ulimruhusu huyu mtu kuchukua moyo wangu najuta kukutana naye
[F] Amepoteza furaha ya moyo wangu, ameharibu udhamani wa maisha yangu, msambaratishaji wa ndoto yangu.
[g] Adui wa maisha yangu mpinzani wa maendeleo yangu.
Haya maombolezo yanapozidi kuendelea mtu huyu anaamua kufanya maamuzi ambayo wengi hawataweza kukubaliana nayo, ila yupo kwenye harakati ya kujiokoa nafsi yake hata kufikia kuchukia kupenda au kupendwa maana teso alilopata ni kubwa sana wewe usifanye unajua sana kuongea hujui teso la mapenzi hujui moyo wa mtu ulivyoumizwa – usidanganyike na muonekano wake – aliyeumia yupo.
Unaweza kumuona amelala kitandani na wakati mtu wa ndani amekaa kwenye mkeka anamsiba mkubwa,
[a] Machozi hayamuishi
[b] Mawazo yamemsonga sana,
]c] Moyo umesafiri haupo pale,
[d] Kazi haziendi,
[e] Huduma yake inazidi kuharibika kila siku,
[f] Afya inakwisha kila siku,
[g] Ofisini haonekani kazini anakuja lakini nafsi yake haipo pale na hata wengine wanaweza kutambua kuwa mwenzetu hayupo hapa.
Unaweza kuongea na mtu ambaye nafsi yake ipo nyumbani kwake sio mchezo. Hapo ndio chanzo cha Msongo wa mawazo hutokea, moyo ulioumizwa kimapenzi unahitaji uangalifu sana kuutibu na kuushauri. Wachungaji wengi wamechangia ndoa za wengi kuvunjika kwa kutokuwa na ufahamu mkubwa wa upendo na matokeo yake, usiwe mwepesi wa kutoa maandiko mengi wakati hujui mateso ya mapenzi najua kuwa unajua kuwa mapenzi ni sumu, yanapoharibika hutakiwi kuwa mwepesi kuyaingilia maana mapenzi yamebeba maisha ya mtu,
Unapotaka kumshauri mtu aliyeathirika na mapenzi unatakiwa kuyafahamu mambo haya muhimu nayo ni:-
1. Unatakiwa kujua maana ya upendo na gharama zake.
2. Lazima ujue vyanzo vya kujenga uhusiano ili uwe imara na mwenye nguvu katika maisha ya wapendanao.
 3. Mambo 32 yanayojenga uhusiano kama ulivyosoma.
4. Lazimaujue mambo yanayoweza kuharibu mahusiano na milango ya kuvunja mahusiano.
5. Lazima ujue maumivu ya mapenzi ili uweze kuwaponya waliojeruhika kimapenzi.
Nina maswali ya kujiuliza kuhusu UPENDO jambo hili ni kubwa sana katika maisha ya mwanadamu hakuna asiyejua maana limechukua sehemu kubwa katika MOYO wa mwanadamu,watu wengi tumekuwa tunalia sana, tumekuwa tunakata tamaa,tumekuwa tukigombana, hata hatua ya kuumizana na wengi wamekufa na wengi hawataki kupenda tena. Na kundi lingine linasema kupenda ni mzuri sana wanasema unanguvu sana na wakati mwingine wanasema kupenda ni kifo na wanaona unakupeleka jehanamu katika sehemu saba zifuatazo:
1. Sehemu ya mateso
2. Sehemu ya mahangaiko
3. Sehemu ya masikitiko
4. Sehemu ya magomvi
5. Sehemu ya matukano
6. Sehemu ya kudhalilishwa
7. Sehemu ya kuchafuliwa
Kwa nini tunapenda na kwa nini tunatumia ikiwa upendo ni mzuri Ni nani anayesababisha nipende na ninanianyenipenda kweli? Ni ninani nitayempenda? Na kwanini upendu unanguvu na imechukua sehemu kubwa ya maisha yangu? Sasa upendo ni nini na inamaana gani?
ZIPO AINA SITA [6] ZA LOVE
1. Philotheos - upendo wa mungu; 2timoth 3:4
2. Philoxenos - kupenda wageni [ xenia…..hospitality
3. Philagathos - kupenda kitu kizuri; titus 1:8
4. Philarguros - kupenda pesa; luke 16:14 and 2timoth 3:2
5. Philautos - kumpenda mtu mmoja; 2timoth 3:2
6. Philedonos - kupenda starehe; 2timoth 3:4
Unajua ni vizuri sana kama utapenda mahali unapopendwa kuliko kupenda mahali usipopendwa, unatakiwa uwe na ufahamu mkubwa sana wa mapenzi kabla ya kuyaingia unaweza kupoteza ndoto zako za maisha, maaana mapenzi yanauwezo mkubwa sana wa kuharibu maisha yako. Mabinti wengi na vijana wamejikuta wameingia katika mchezo huu wa mapenzi wakiwa na akili za kitoto huku wakijua kuwa upendo ni kitu cha kawaida leo wanalia sana kutokana na maumivu waliyoyapata. Rafiki yangu ningependa nikwambie Upendo ni nini ?
1. Upendo ni mzuri sana kama utajua maana na kusudi la Mungu kuweka pendo ndani ya mtu.
2. Upendo unatesa
3. Upendo unaua
4. Upendo unakondesha
5. Upendo unaharibu maisha
6. Upendo unaharibu utaratibu wa mtu
7. Upendo unanyonga maisha
8. Upendo unaathiri akili ya mtu
9. Upendo ni gharama
10. Upendo ni shule
11. Upendo ni maisha ya mtu.
Mpendwa wangu neno hili (Upendo) sio kitu cha mchezo, wewe unaweza kuwa ni mtoto, mwanafunzi hujajipanga bado utaratibu wako wa maisha unatakiwa uwe makini sana katika jambo hili, unajua kuwa Upendo unauwezo mkubwa sana wa kutoa ufahamu wa mtu na kuharibu utaratibu wa mtu? Upendo unapoingia ndani ya moyo mtu anauwezo mkubwa wa kukutoa katika mipango yako, upendo ukikolea watu wanauwezo wa kusahau familia zao, masomo, kazi zao, na utaratibu wake wa kila siku unaharibika, upendo unatakiwa kuheshimika na kila mtu unatakiwa kutembea katika upendo kwa unyenyekevu mkubwa, utiifu na adabu maana sio jambo la mchezo, usichukulie jambo hili kitoto unatakiwa unapoamua kufanya maamuzi ya kupenda au kupendwa unatakiwa uwe na maswali (14) hayo ya msingi ili usije kuumia kama sisi tulivyoumiza na kuumizwa bila kujua, maana yake na gharama yake.
MASWALI KUMI NA NNE (14) YA KUJIULIZA KABLA YA KUCHUKUA UAMUZI WA KUPENDA NA KUPENDWA
1. Kwa nini ninapenda?
2. Upendo ni nini?
3. Je huyu anayenipenda anajua maana ya kupenda?
4. Je amenipendea nini?
5. Je ana malengo gani juu ya maisha yangu?
6. Amejipanga vipi juu ya makwazo yatakavyo jitokeza baadaye?
7. Je amenipenda love au ananitamani LIKE?
8. Je ana ujasili wa kukabiliana na mazito mbeleni katika maisha?
9. Je yupo tayari kunishika, kuniongoza, kunishauri, kunifundisha nisiyoyajua, atakuwa na muda na mimi na ataniombea?
10. Je ataheshimu mawazo yangu na hisia zangu?
11. Je ni mcha Mungu? Na anamuelekeo juu ya MUNGU?
12. Je historia yake ikoje na ametoka wapi?
13. Je kuna mipaka ipi katika upendo wetu?
14. Je ameathika kweli juu yangu?
KWA NINI TUNAPENDA NA TUNAPENDWA?
Hakuna anayependa bila sababu na hakuna anayependwa bila sababu zinazomfanya.
Mtu kupenda au kutopenda hata Mungu alikuwa na sababu za kuupenda ulimwengu hata
Kumtoa mwana wa pekee ulumwenguni. Kupenda sio dhambi na kutopenda sio dhambi.
Upendo ni ssehemu ya maisha na ni Mungu ambaye ameweka kwa mwanadamu Hivyo.
Upendo umetoka kwa Mungu sio mtu ameamua kupenda jua kuwa upendo ni sehemu ya maishsa hata wanyama wanapenda na wana wivu wao kwa wao lakini upendo wa mwanadamu ni kubwa na unanguvu kuliko wanyama sababu nilizo nazo kwanini ninapenda na kwanini ninapendwa na ninani natakiwa kumpenda?
(1) Kwa sababu naitaji kufarijiwa [nafsi]
(2) Kwa sababu naitaji kukamilishwa [mwanz 2;18-]
(3) Kwa sababu upendo ni nature
(4) Kwa sababu ni mpango wa Mungu
(5) Kwa sababu nahitaji kupendwa
WATU WALIOSAHIHI WANAPATIKANAJE.
Najua unaweza ukawa na swali kama hili, kutaka kujua nitawezaje kupata mume sahihi au mke sahihi katika maisha yangu?
Jibu ni kwamba Mume au Mke aliye sahihi katika maisha yako “anatengenezwa na wewe mwenyewe na hili siyo kazi ya Mwanaume kama baadhi ya watu wanavyofundisha bali ni kazi ya watu wawili wanaopendana Mwanamke na Mwanaume. Mtu sahihi anaandaliwa mapema maana hata waswahili wanasema “Samaki mkunje angali mbichi” unajua hakuna timu nzuri kama haina wakufunzi wazuri. HIVYO:
a) Mapenzi yanalelewa.
b) Mapenzi yanatafutwa bila kuchoka.
c) Mapenzi yanaandaliwa.
d) Mapenzi yanapaliliwa (Kama shamba).
e) Mapenzi yanatunzwa.
f) Mapenzi ni shule kila siku.
g) Mapenzi Yana mfano wa yai, yanashikwa kwa uangalifu wa hali ya juu sana, hayachuliwi na mtu mwenye akili za kitoto.
h) Lazima ujue uthamani wake na umuhimu wake katika maisha ya mwanadamu.
i) Mapenzi ni maisha yetu ya kila siku tuliyonayo.
j) Mapenzi yanaishi ndani mtu aliyekubali kujifunza.
k) Mapenzi ni matamu sana ukiyapatia
l) Mapenzi ni machungu sana ukiyakosea.
m) Mapenzi yanakaa kwa mtu anayetamani mabadiliko katika maisha yake.
n) Mapenzi ni uzima katika moyo wa mtu akiyapatia.
o) Mapenzi ni mauti na majuto ukiyakosea.
p) Mapenzi yanaharibu heshima katika jamii ukiyakosea.
q) Mapenzi yanaleta heshima katika jamii ukiyapatia
r) Mapenzi ni kitabu kinachosomwa na kila mtu mdogo na mkubwa.
s) Mapenzi ni bustani nzuri sana inayotengenezwa na mtu, analima, anapanda, anamwagilia maji na kuipalilia.
t) Mapenzi ni maneno matamu yanayoweza kutekenya moyo wa mtu yasiyoweza kumboa mwenzi wako, yakumfanya afurahi, akijisikia kuheshimika, kutambulika, kukubalika, kuthaminika na kupendwa.
u) Mapenzi hayana kiongozi bali katika mapenzi tunaongozana sisi kwa sisi..
v) Katika mapenzi kila mtu anatakiwa kuwa kioo cha mwenzi wake, mrekebishe, mtengeneze, mfanye akubalike katika jamii iliyokuzunguka.
w) Matengenezo ya mapenziyanahitaji muda (time) ya kutosha na mwenzi wako ukiwa na muda wa kutosha utaweza kumfahamu mwenzi wako akichukia anakuaje? Anapofurahi anakuaje? Hata kama kuna wengine huficha makucha yao unatakiwa kuto mitihani ili kufanya (teste) maana hakuna masomo yanayoweza kujifunza yakakosa mithani..
x) Mtihani ni kipimo tosha cha kugundua uelewa wa mtu au mwenzi wako kuwa mtafika katika safari hiyo ya mapenzi au usitishe kutoendelea na safari.
y) Mapenzi ni hadithi nzuri sana iliyokuwa na “mkato (,) nukta (.) na kiulizo (?)
z) Mapenzi ni utiifu, unyenyekevu, upole, usikivu, na matendo.
Mpendwa wangu ukiyajua hayo unaweza ukapata Mume au Mke mzuri sana katika maisha yako, mtengeneze mtu mwanzoni kabisa mwa mapenzi yenu kabla mapenzi hayajakomaa na kuota mizizi. Mimi Silvester Paulo niliyakosea mwanzoni niliumizwa sana, yakaharibu mfumo wangu wa maisha yangu. Hivyo nimewahi kuumizwa kimapenzi ijapokuwa ni Mtume, Mchungaji, mapenzi hayaangalii VYEO (TITLE) ulichonacho. (Mapenzi ni kitendawili kisichoweza kuteguliwa)” Huu ndio msemo wangu” Leo nimekuwa mwandishi wa vitabu na mwalimu baadaya kujifunza kivitendo. Mapenzi ni watu wawili tu na watatu ni Mungu msipoweza kusikilizana ninyi hakuna atakayeweza kukusaidia. Mtengeneze mwenzi wako kwa bidii sana kwa kuwa na muda naye wa kutosha, ukimfundisha, kumonya na kumuombea kwa Mungu ili aweze kuwa mtu wa kufaa kimaisha maana kuumizwa kimapenzi ni kuumizwa kimaisha
UPO UWEZEKANO WA KUPATA MTU ASIYE SAHIHI KATIKA MAISHA YAKO
Upo uwezekano mkubwa sana kuumizwa kimapenzi kutokana na tabia tofautitofauti na migongano isiyoweza kuepukika na inayoweza kuepukika.
Mwanamke na Mwanaume sahihi kumpata sio mchezo ni historia maana mapenzi ya kweli ni “UTUMWA” mapenzi ya kweli yanatesa moyo wa mtu.
JINSI YA UPATIKANAJI WA MTU ASIYE SAHIHI KATIKA MAISHA
1. Hutumia hila wakisema kuwa Mungu amenionesha kuwa wewe ni mke au mume wangu hili ni moja ya njia wanapatikana madada wengi na wa kaka waliookoka.
2. Wanatumia pesa zao wakijifanya wanakusaidia, wanakujali sana, wanakuthamini na kukuheshimu – kwamba wanakutafuta ili wayaumize maisha yako hawana mapenzi ya kweli.
3. Wanatumia maumivu yako ya mapenzi Kama silaha ya kukupata.
Mfano:
Umewahi kutendewa mabaya na mwenzi wako uliyekuwa unampenda sana akakuumiza moyo huwa sasa wanajifanya kuwa ni
a. Wafariji wa moyo wako.
b. Waponyaji wa majeraha yako.
c. Washauri wa karibu.
d. Wanajionyesha kuwa wao wanajua mapenzi kuliko yule.
Kumbe wanataka kutumia nafasi hiyo kukupata na wengi wamepatikana wanaumizwa zaidi.
4. Wanatumia hali mbaya uliyonayo ya uchumi kifamilia kama njia ya kukupata wanatumia mambo yafuatayo:-
a. Wanakutafutia mtaji- pesa, biashara nk.
b. Wanaweza kuanza kulisha familia yako.
c. Wazazi wako watatuzwa.
d. Kununuliwa mavazi, chakula, afya yako, hata wanaweza kukujengea nyumba, kukununulia magari kumbe ni wauaji wa ndoto zako. madada wengi wamedanganyika na vijana wengi leo wanajutia.
5. Wengine wanaingia kwa kishindo cha penzi la kweli kumbe lina unafiki ndani yake – muangalie Delila alivyomuingia Samsoni kumbe hakuwa na penzi la kweli alitafuta kujua siri ya nguvu za Samsoni na kumuangamiza wengi tumeumizwa hivyo kumbe mapenzi ni shule kubwa sana kila siku tunajifunza hakuna aliye mzoefu hata mmoja hasa swala hili la mapenzi Msemo nilionao kuhusu mapenzi Silvester Paul ni huu
“TESO KUBWA SANA KATIKA MAISHA YA MWANADAMU NI KUMPENDA MTU ASIYE SAHIHI KATIKA ENEO LILILOSAHIHI”
YAPO MAMBO 25 YANAYOJITOKEZA:
1. Mtu asiye sahihi huleta mahangaiko na mateso.
2. Mtu asiye sahihi huleta majuto katika maisha.
3. Mtu asiye sahihi huleta umasikini, taabu na maumivu.
4. Mtu asiye sahihi huleta magonjwa ya moyo.
5. Mtu asiye sahihi huleta roho ya kujichukia.
6. Mtu asiye sahihi huvuta roho ya mauti ndani ya mtu.
7. Mtu asiye sahihi huleta kilio kisichoisha ndani ya moyo wa mtu.
8. Mtu asiye sahihi huleta kudharauliwa na matukano katika maisha yako.
9. Mtu asiye sahihi huharibu heshima yako katika jamii.
10. Mtu saiye sahihi huleta ogomvi usioisha katika familia.
11. Mtu asiye sahihi hana toba ya kweli katika maisha yake.
12. Mtu asiye sahihi anauwezo wa kukufanya uchukie kupenda na kupendwa katika maisha yako.
13. Mtu asiye sahihi huleta ugumu wa maisha.
14. Mtu asiye sahihi hupoteza maana yako ya kuishi na kusudi lako.
15. Mtu asiye sahihi huondoa furaha na amani katika maisha yako.
16. Mtu asiye sahihi anaharibu mtazamo wako wa kesho (future).
17. Mtu asiye sahihi anakukosesha na watu walio sahihi maana ana roho za uongo, fitina, unafiki,wachoyo na rafiki wa maadui zako – mwangalie Delila akiwa na urafiki na wafilisti ambao walikuwa maadui za Samsoni Yuda Iskarioti anakuwa na urafiki na watu wenye uadui na Bwana Yesu.
18. Mtu asiye sahihi anakutenga na Mungu wako.
19. Mtu asiye sahihi anaweza kukufanya kupoteza uaminifu wako katika jamii na kufanya mambo yasiyostahili kama kutoka nje ya ndoa, kutoa talaka na kuwachukia watu jinsia Fulani kama wanaume au wanawake.
20. Mtu asiye sahihi analeta maangaiko na mateso katika jamii
21. Mtu asiye sahihi huleta sifa mbaya katika mazingira ya sifa njema.
22. Mtu asiye sahihi huleta mipasuko na migongano katika familia.
23. Mtu asiye sahihi hukwamisha ndoto za watu kutimia.
24. Mtu asiye sahihi huharibu utaratibu wa maisha yako.
25. Mtu asiye sahihi huvuta hofu, woga na mashaka katika eneo zima la kupenda na kupendwa katika maisha yako.
HAZINA ZILIZOWEKWA CHINI YA ARDHI MIILI ILIYOZIKWA CHINI YA ARDHI ZILIZOWEZA KUTIMIZA NDOTO ZAO KWA SABABU YA KUWA NA WATU WASIO SAHIHI KATIKA ENEO LILILO SAHIHI
Kuna watu wamekufa kwa sababu ya maumivu na mateso ya mapenzi, kusalitiwa, kutendewa vibaya na watu waliokuwa wanapenda kumbe walikuwa ni “Mbegu isiyosahihi katika eneo lililosahihi”.
Wengine walikunywa sumu, wengine walijipiga risasi wakafa, wengine walijinyonga, wengine waliuawa maana walikuwa wanatafuta kitu sio penzi la kweli.Kuna miili mingi leo imezikwa hawajatimiza ndoto zao baada ya kupata watuwasio sahihi katika maisha yao. Wewe mwenyewe msomaji wangu unaushahidi mkubwa wa watu walio kufa kwa sababu ya mapenzi, katika Biblia unamuona Uria aliyekuwa mwanajeshi mkubwa tu katika serikaliya Mfalme Daudi siku moja Daudi alikuwa emepumzika juu ya gorofa yake kuangalia chini akamuona mke wa Uria anaoga akamtamani, akatuma wajakazi wake wakamlete ndani akamchukua na kulala naye alivyoona kuwa anamfaa akapanga mbinu jinsi Ulia afe ili aweze kumchukua yule mwanamke moja kwa moja akawaambia nendeni vitani na Uria mtangulizeni mbele ili afe, mbinu yake ikafanikiwa Uria akafa kabla ya ndoto yake kutimia unajuje kama angeweza kuwa mtu mkubwa sana baadaye mapenzi yanaweza kukwamisha ndoto za watu wengi sana.

No comments:

Post a Comment

Pages