IFAHAMU NJIA BORA KULIKO ZOTE YA KUZUIA MIMBA KWA UZAZI WA MPANGO. - MrPeacePaul
IFAHAMU NJIA BORA KULIKO ZOTE YA KUZUIA MIMBA KWA UZAZI WA MPANGO.

IFAHAMU NJIA BORA KULIKO ZOTE YA KUZUIA MIMBA KWA UZAZI WA MPANGO.

Share This
   
Elimu ya uzazi wa mpango bado haijawafikia vijana wengi sana hasa tanzania, wengi wao hudhani labda
matumizi ya dawa na njia za uzazi wa mpango ni kwa ajili ya malaya, watu waliokwisha zaa na kadhalika. lakini hii sio kweli kwani njia hizi ni nzuri kwa rika zote yaani vijana na watu wazima ambao wanashiriki ngono ila kwa sasa hawako tayari kupata mtoto.

kutotumika kwa njia hizi kumesababishwa kuzaliwa kwa watoto wengi ambao hawakupangwa, kujiua kwa wasichana kwa kukwepa aibu na utoaji wa mimba wa mara kwa mara.
utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba msichana akiingia kwenye mahusiano kwa miaka mitatu bila kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango anaweza kutoa mimba nne mpaka tano lakini pia asilimia kubwa ya wanachuo wa tanzania ambao huingia kwenye mahusiano vyuoni hawawezi kumaliza chuo bila kutoa mimba hata moja.

kuna njia nyingi sana za uzazi wa mpango ikiwemo vitanzi, vijiti, kondomu,kutumia kalenda, sindano,vidonge, upasuaji wa kufunga mirija na kadhalika. kondomu ni njia bora sana kwani huzuia ukimwi na mimba pia lakini ukweli ni kwmba kama kondomu zingekua zinatumika vizuri basi hao watoto tusingewaona mtaani hivyo kama wewe hauko tayari kuzaa sasa hivi kwa sababu yeyote ile nakushauri utumie njia ya kijiti.

njia hii ikoje?
kijiti cha plastiki chenye homoni za uzazi huwekwa kwenye mkono wa mwanamke, homoni ndani ya kijiti hicho huzuia mimba kwa kwa kuzuia yai kutoka kwenye kiwanda yaani ovari kwenda kwenye kizazi . kijiti hiki huwekwa bure kwenye hospitali zote za serikali tanzania.

kwanini njia hii ni bora kuliko zote?

hurudisha uwezo wa kuzaa haraka: kama unatumia kijiti hata kama kiliwekwa wiki iliyopita, ukibadilisha mawazo ukataka mtoto kinatolewa na mwezi huohuo unapata mtoto, tofauti na njia ya sindano ambayo ukichomwa leo kuna uwezekano wa kukaa mpaka miaka miwili bila kupata mtoto.

ni rahisi kutumia: kijiti hiki kikishawekwa hospitali huhitaji kukumbuka chochote tofauti na vidonge ambavyo wakati mwingine mtu huweza kusahau asimeze akajikuta amebeba mimba.

inafanya kazi kwa muda mrefu sana; kama wewe ni binti mdogo au wewe ni mama ambaye una mtoto tayari na hauhitaji mtoto kwa sasa njia hii ni nzuri kuliko zote kwani huweza kuzuia mimba kwa miaka mitano mfululizo kwa asilimia mia.

haiingilii utoaji wa maziwa ya mama; vidonge vya uzazi wa mpango vyenye homoni zote mbili yaani oestrogen na progesterone kitaalamu kama microgynon huweza kupunguza wingi wa maziwa kwani wingi wake kwenye mfumo wa binadamu husababisha kupungua kwa homoni ya maziwa kitaalamu kama prolactin hormone.

haiongezi uzito; inaaminika vidonge vya uzazi wa mpango huongeza uzito kwa kuzuia kiasi kikubwa cha maji kisitoke ndani ya mwili kwa njia ya mkojo na pia kuongeza hamu ya kula, lakini utafiti kwa wanaotumia vijiti haujaonyesha madhara haya.

muda zaidi wa kushiriki tendo la ndoa: matumizi ya kijiti huzuia kutoka kwa damu ya kila mwisho wa mwezi ambayo kwa wengine huambatana na maumivu makali na kukosa raha ya kushiriki tendo la ndoa hivyo ukitumia kijiti utapata faida hii.damu inaweza ikatoka hata mara mbili kwa mwaka tu.

sio rahisi kwa watu wengine kujua: wasichana wengi hasa vijana hawapendi maisha yao ya ngono yafahamike, na hasa njia hizi za uzazi wa mpango watu wakijua unatumia wanakuona muhuni, kitu ambacho sio kweli, hivyo matumizi ya kijiti ni siri sana na sio rahisi kwa watu wengine kujua tofauti na vidonge ambavyo sio rahisi kuvificha.

mwisho; utafiti unaonyesha utoaji wa mimba umewanyima wanawake wengi watoto, msanii maarufu wema sepetu ambaye kwa sasa anatafuta mtoto kwa shida sana aliwahi kukiri kwamba aliwahi kutoa mimba zamani kidogo na huenda anajutia maamuzi yake.hivyo kama wewe ni msichana mdogo na hutaki kuzaa kwa sasa au wewe ni mama hutaki mtoto mwingine kwa sasa tumia njia hii ya uzazi wa mpango itakusaidia sana.

No comments:

Post a Comment

Pages