Moja Ya Jambo La Kuzingatia Ili Kuboresha Mahusiano Yetu Na Wengine. - MrPeacePaul
Moja Ya Jambo La Kuzingatia Ili Kuboresha Mahusiano Yetu Na Wengine.

Moja Ya Jambo La Kuzingatia Ili Kuboresha Mahusiano Yetu Na Wengine.

Share This


downloadwwwwwwwwwwwwwwww
Kuna mtu mmoja alisema “ukiona hauhitaji watu ili kutimiza ndoto yako, basi ndoto yako ni ndogo. Kama una ndoto kubwa lazima utahitaji mchango wa watu wengine”.  Safari ya mafanikio inahitaji watu. Bila masaada wa watu wengine itakuwa ngumu sana kutimiza ndoto zako kubwa.
Uhusiano wetu na watu wengine ni moja ya jambo muhimu sana kwenye safari yetu ya mafanikio. Bila kuwa na uhusiano mzuri na wengine, lazima tutakwama  njiani kwenye safari yetu ya mafanikio.
Illi tuwe na mahusiano mazuri na wengine kuna kitu kimoja ambacho tunakiwa kukizingatia. Kitu hiki tunatakiwa kukipa kipaumbele kuanzia tunapofanyia kazi mpaka nyumbani. Kitu chenyewe ni kuwaona wengine ni bora kuliko sisi.
Kuwaona wengine kuwa ni bora, haimaanishi kwamba wewe sio bora na wala haimaanishi kwamba hujui. Kuwaona wengine ni bora, inamaanisha kujishusha na kuona thamani na uwezo ambao umo ndani yaw engine.
Watu wengi tunapenda kuonekana kwamba sisi ni bora kuliko wengine. Tunapenda kuonekana kwamba tunajua sana kuliko wengine. Mara nyingi tunapoana wengine wanafanya kitu  kwa ubora na kutuzidi uwa tunaumia.
Mafanikio kwenye mahusiano yako na maeneo mengine yanaanza kwa kuwaona wengine ni bora kuliko wewe. Huwezi kufanikiwa kama kila siku unajiona wewe ni bora sana kuliko wengine.
Hakuna binadamu anayependa kushushwa. Unapowashusha wengine na kuwaona sio bora na wao lazima watakushusha. Kama unataka wengine wakuone wewe ni bora, basi anza kuwaona wengine ni bora kwanza.
Waone wengine ni bora.  Wakubali wengine jisi walivyo na wape thamani na uone uwezo mkubwa uliomo ndani yao. Usiwadharau wengine na kuwaona kwamba  sio bora kama wewe. Kila mtu ana ubora wake. Kila mtu ana uwezo mkubwa ndani yake.
Kila mtu ana umuhimu wake na ndio maana yupo duniani. Kama uoni umuhimu wake kwako, yeye ni muhiumu kwa watu wengine.  Sio tabia ya wanamafanikiokuwashusha wengine na kujiona  ni bora sana kuliko wengine.
Ni jukumu letu kuwaona wengine ni bora na wana uwezo mkubwa ndani mwao wa kufanya makubwa. Mafanikio yanaanza kwa kuwaona wengine wanaweza na kuwahamasisha kuona na kutumia uwezo wao mkubwa na sio kuwashusha na kuwaona hawawezi.
Tafakari njema rafiki yangu.

No comments:

Post a Comment

Pages