(MAHUSIANO) hizi ndizo faida kuu 2 za kutoa zawadi katika mahusiano ya mapenzi.... - MrPeacePaul
(MAHUSIANO) hizi ndizo faida kuu 2 za kutoa zawadi katika mahusiano ya mapenzi....

(MAHUSIANO) hizi ndizo faida kuu 2 za kutoa zawadi katika mahusiano ya mapenzi....

Share This


1.   ZAWADI ZINABORESHA MAPENZI:
Umuhimu wakwanza wa Zawadi katika mapenzi ni kuboresha mapenzi. Fahamu kuwa unapompa mpenzi wako zawadi utamfanya ajihisi kama niwapekee kwako hivyo atajiona kama ni mmoja wapo kati ya watu wenye thamani kwako na ataamini kama kweli upo karibu yake na unamjali hivyo hatashindwa kulipa mazuri kwako kwa kukuonesha upendo wa dhati na utamfanya azidishe mapenzi kwako kwani atakua anajua kuwa wewe unamjali na unamuonesha upendo sasa kwanini nayeye asikujali?! Hivyo zawadi yako itakuwa ni njia moja wapo ya kuboresha penzi lako kwa umpendae.

2. ZAWADI ZINAJENGA KUMBUKUMBU KATIKA MAPENZI:Umuhimu wa pili wa zawadi katika mapenzi ni kujenga taswira ya kumbukumbu kwa mpenzi wako, faham kuwa unapompa mpenzi wako zawadi inakusaidia wewe kujijenga katika mawazo yake na endapo kama itatokea mkaachana nae basi pindi mpenzi wako atakapokuwa anaziona zawadi zako zitamfanya akukumbuke kwa mengi na atahisi kama kuachana nawewe kwake kunatofauti na atajihisi kupoteza vingi toka kwako na kamwe kumbukumbu yako kwake haitofutika kila azionapo zawadi zako.

No comments:

Post a Comment

Pages