NJIA 7 NZURI ZA MAWASILIANO KATIKA MAHUSIANO YAKO: - MrPeacePaul
NJIA 7 NZURI ZA MAWASILIANO KATIKA MAHUSIANO YAKO:

NJIA 7 NZURI ZA MAWASILIANO KATIKA MAHUSIANO YAKO:

Share This
Kuna aina nyingi za mahusiano, yapo ya kirafiki, ya familia, ya kazini, kwenye mahusiano ya mwanamke na mwanaume na hata mahusiano ya mwanamke na mwanamke na ya  mwanaume na mwanaume yapo.
kila mmoja anamahitaji yake ya kipekee  yanayomuelezea yeye kuwa  ni mahusiano gani  alionayo. na ukumbuke binadamu tunahitaji kuelewana ili kuziimarisha roho zetu na miili yetu.lakini ukweli ni kwamba , kukosekana kwa mahusiano mazuri  humaliza  akili za watu na nguvu pia.
Hasa pale panapokuja swali gumu  la mawasiliano.
Kwa ufupi  sifa ya kila mahusiano hushushwa na sifa ya  mawasiliano.

Inabidi kujifunza kuwasiliana ambapo ndio njia nzuri ya kutengeneza mahusiano bora  badala ya mvurugano uliopo kwa kila mtu. na hapa kuna njia zifuatazo za ufanisi ya mawasiliano  bila ya kujali yale mahusiano ya ana kwa ana.
1.Jifunze kutulia.
02-powerful-body-language-watch-partners-mouth-1024x682 NJIA 7 NZURI ZA MAWASILIANO KATIKA MAHUSIANO YAKO:
Mruhusu mtu unaewasiliana nae kuongea jinsi anavyojisikia,  na atoe mawazo yake bila ya wewe kumuingilia. vaa kiatu chake wakati huo unaposikiliza,  hapo unaposikiliza hutakuwa tu unamwelewa bali utakuwa unajifunza na kupata uzoefu na uwelewa mzuri zaidi.
2.Jifunze kuwa msikilizaji mzuri.
Fanya kama wewe umealikwa , na unataka kuwasikiliza watu wanaowasiliana. lakini usije ukakaa tu bila ya maswali. jitahidi kuuliza maswali mengi ili kuongeza hari ya huyo mzungumzaji aendelee  kuongea, na wakati huo usitegemee majibu , ila  kumbuka kuwa uko kwenye mawasiliano ya namna gani. uwe makini na hilo ili usitoke nje ya mstari.
3.Wengine huvuta hisia za mwanzo.
Pamoja na kwamba utaweka nguvu ya kusikiliza , bado kuna watu  wanaopenda kukumbushia yalipita ili kuleta kitu cha kutoelewana. wewe unyesha kujali bila kuogopa hayo.baadae yeye mwenyewe ataona haina haja ya kubaki na haya, na utaona itachukua muda mfupi tu kuelewana. ni hatari lakini salama.
4.Usipanic, usifanye papara.
Mawasiliano yanapoendelea usiingilie muda, subiri mpaka huyo mtu amemaliza kuongea na kujieleza. kama utaona bado hayuko tayari kusikiliza,  haijalishi  una neno zuri  la namna gani la kuongeza, ndugu ujumbe wako hautafika.kwa hio subiri tu.
5.Usijaribu kuongea juu ya mtu mwingine.
Kama ulikuwa unaongea na ukaona  umeingiliwa katika maongezi yako , tulia,  usijaribu kuongea juu ya mtu mwingine, yaani mtu anaongea na wewe unaongea , usifanye hivyo. hatakujibu hata hivyo labda awe ni mtu wa ovyo, lakini kama hataweza   kusikiliza mwambie kuwa umeharibu mawasiliano.
6.Wasaidie wengine wawe wasikilizaji wazuri pia.
hii hapa inafanyika hivi, kama  umewaeleza kitu  uliza endapo wamekuelewa ulichowaambia, na wakueleze ulichokisema. na hapa ndipo utakapojua kuwa kuna wasikilizaji ama hakuna,lakini usiache kuwaelewesha  mpaka wamekuelewa.
7.Usihofie ukimya wa muda.
201207-orig-relationship-949x534 NJIA 7 NZURI ZA MAWASILIANO KATIKA MAHUSIANO YAKO:
mawasiliano ya kibinadamu ni rahisi sana kuliko kuongea maneno. wakati wa ukimya ndio wakati mzuri wa mawasiliano, hata hivyo katika hali nyingi za mawasiliano ya ukimya  unawafanya watu wasijiamini, wasitulie.
Lakini kumbuka kuna watu wanahitaji ukimya ili wakusanye mawazo yao ili wawe salama kuongea kitu cha msingi. na wakati huo wa ukimya unatakiwa kuwa msikilizaji mzuri zaidi ya wakati wa kuongea.

shirikisha familia na marafiki ujumbe  huu mzuri. na nakukaribisha utoe maoni yako.

No comments:

Post a Comment

Pages