Kwenye kiasi na sifa inapofanya tofauti.
Kuridhika kwenye mahusiano sio kitu pekee ambacho kinatupatia furaha ya kweli, yanashawishi afya ya muda mrefu pamoja na kupata muda wa kutosha wa kulala, kula chakula chenye afya, na bila ya kuvuta sigara au ulevi wa pombe.
Utafiti wa wachunguzi umegundua kuwa kuridhika ndani ya mahusiano inaletwa na afya njema, furaha ya kutosha, na hata maisha ya muda mrefu.
Athari hii sio ndogo kwenye mahusiano ya kimapenzi—marafiki wa karibu na uhusiano wa kijamii kwenye familia na washiriki wa jumuia pia wanaweza kusaidia afya hio.
Sifa ya mahusiano inaweza kuleta utofauti?
Kiasi kikubwa katika jamii kinapofanya tofauti kwenye uhusiano, sifa pia inakuwepo.
Watu wenye umri wa kati wanapokuwa na mahusiano mazuri kwenye ndoa , uwezekano wa kuepukana na magojwa ya moyo, kiharusi ni mkubwa kuliko wale ambao wana uhusiano mbaya ndani ya jamii na katika mahusiano yao ndani ya ndoa.
Mahusiano yakiwa ni mabaya kwenye familia , marafiki pia inaweza kuleta stress na kuharibu afya, mambo ya kisukari, moyo mkubwa, hizi hisia za kimwili na hali ya akili inakuwa kwenye hatari ya magonjwa.na hii yote inatokana na msongo kupita kiasi.
Wenza wetu wanatuhamasisha kuishi kwa afya njema?
Kuwa katika mahusiano yenye kusaidiana inatuwezesha pia kushawishika kuishi maisha yenye afya.Jamii inasaidia kuhamasisha watu kula mboga za majani za kutosha , kufanya mazoezi, na kuacha kuvuta sigara. Kama utakuwa na watu wenye kujua afya ni nini itatusaidia hata sisi kujali afya zetu.Au tunaweza kuhamasika kufanya mazoezi pamoja na marafiki, wenza na wengine. Mke anaweza kutengeneza chakula chenye sifa ya kuleta afya ndani ya familia ili tuishi vizuri.
Kuna tofauti kati ya kumtia moyo mtu na kumtawala,. Mwenza kumsaidia mwenzake katika kuelimika badala ya kutaka kumbadilisha tabia kwa kumtawala. Tabia ya kuwa na msaada ni akili yenye afya, wakati huo huo kutawala tabia ya mtu ni kuharibu afya ya akili.
Kama tunaweza kuwaza mazuri na kuwa wenye huruma na wenye moyo uliowazi, tunaweza kuwasaidia wenza wetu kufikia malengo ya afya njema, na kuishi maisha mazuri yenye afya ya upendo.
Jamii inatusaidia kuondokana na mwitikio wa msongo?
Jamii inasaidia kupunguza kuwa na misongo ya maisha . kwa kuongea wazi , tunapoongea na marafiki wa karibu, familia. Inaonekana kuwa hawa watu ambao huongea matatizo yao hupata nafuu au kuepukana kabisa na msongo uliopo na hatimae kuepukana na magojwa ya moyo, kisukari , kuliko wale ambao hawajihusishi na jamii.
Vipi kuhusu Huzuni?
Hatari ya huzuni kwa watu, msaada wa mahusiano unaweza kuwa ni jibu kubwa. Unapokuwa na msaada mzuri kwenye jamii uliopo huzuni , magonjwa ya moyo na kisikari hayatakuwepo. Watu wenye msaada wa kutosha hufanya kazi nzuri na wana afya njema. Kwa mfano katika kuleta mabadiliko, afya ya akili inatokana na msaada wa mahusiano,Athari hizi zimekuwepo kwenye mahusiano mengi. Ikihusisha wanafunzi wa vyuo, watu ambao hawana kazi, na wazazi wenye watoto wenye matatizo kiafya.
Mahusiano yana athiri vipi afya yako?
Jamii inatusaidiaje kuwa na afya? Inaonekana ni tabia ya kibaiolojia,na njia ya kihisia , wenza na marafiki au familia wanaweza kututia moyo kwa kutusikiliza , kuonyesha kuwa wanajali,kutusaidia tujifahamu, kutushawishi tuwe na afya njema, au kutuondolea bugudha ya msongo. Kwa njia nyingine , kukosolewa na kuwepo na mambo yanayoendelea ambayo hayana ufumbuzi wa matatizo ambayo yanatufanya tujisikie wenye msongo zaidi na kutuondolea nguvu ya kusimamia matatizo.
Washirikishe wengi wajifunze.
No comments:
Post a Comment