Jinsi shukrani inavyoweza kubadili afya yako
Shukrani inaweza kufanyika kwa kutamka maneno, kutoa fedha au vitu. Zifuatazo ni faida za kiafya ambazo zinaambatana na kushukuru:
Shukrani inaweza kukuongezea uvumilivu
Utafiti wa Chuo Kikuu cha Northeastern kilichopo Marekani ulibaini kuwa watu ambao wanashukuru hata kwa mambo madogo kila siku walikuwa na uvumilivu na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ikilinganishwa na wale ambao hawakushukuru.
Wahitimu 105 wa Chuo hicho waliulizwa kuchagua kupokea kiasi kidogo cha pesa kwa muda mfupi au kupata fedha nyingi kwa siku zijazo; wanafunzi walioshukuru kwa fedha kidogo walizopewa katika majaribio hayo walipata fedha zaidi kuliko wale ambao walikuwa wakitaka fedha nyingi.
Shukrani inaimarisha mahusiano
Kulingana na Jalida la Theoretical Social Psychology linaloangazia saikolojia za watu linaeleza kuwa ikiwa wanandoa watajenga hisia za kushukuru inaweza kuwasaidia kuimarisha mahusiano yao ikiwemo kujisikia wameungana na kuridhika na hali zao. “Kuwa mwenza ambaye anakushukuru wewe na wengine inaweza kuwajengea maisha ya upendo”, anasema Emma Seppala, Mtafiti wa masula ya furaha kutoka Chuo Kikuu cha Stanford.
Shukrani inaimarisha kujipenda na kujithamini
Katika utafiti uliochapishwa katika jalida la Haiba na Tofauti za Watu, ambapo watafiti waliwauliza watu kutoa maoni ya shukrani juu afya ya mwili na akili, kufanya mazoezi, kula chakula bora na kuchunguza afya. Walibaini kuwa kuna mahusiano chanya kati ya kushukuru na tabia zilizotajwa hapo juu, na kupendekeza kuwa kutoa shukrani kunawasaidia watu kujikubali na kuthamini miili yao.
Shukrani inaweza kukusaidia kupata usingizi wa uhakika
“Hesabu Baraka na sio kondoo”, anasema Mtafiti Seppala. Katika utafiti wa Journal of Psychosomatic Research umebaini kuwa kushukuru kunamsaidia mtu kulala vizuri na kwa muda mrefu. Hilo linawezekana kwasababu, “unakuwa na mawazo chanya kabla ya kwenda kulala” anasema Seppala ambaye hakuhusika kwenye utafiti huo na kuongeza kuwa hatua hiyo inakuondolea mawazo mabaya na kuifanya akili kuwa katika hali nzuri ya kufikiri.
Shukrani inaweza kukuzuia kula kupita kawaida
Watafiti wanasema kushukuru kunaongeza uwezo wa kusimamia hisia za ndani na kukusaidia kufanya maamuzi sahihi ya chakula unachopaswa kula kulingana na mahitaji ya mwili.
Shukrani inaweza kukusaidia kupunguza mfadhaiko na huzuni
Susan Thompson, Mwanasayansi wa saikolojia ya ulaji kutoka nchini Marekani anasema ikiwa mtu atakumbuka mambo mazuri aliyoyapata katika kipindi fulani na akashukuru hata kama ana huzuni inaweza kumsaidia kurudi katika hali ya kawaida na kuwa na furaha.
Mtafiti wa Seppala anafafanua kuwa, "Shukrani inakuongoza katika furaha endelevu kwa sababu haitokani na tukio la mara moja bali imejikita kwenye akili". Ikiwa utajenga mazoea ya kushukuru kwa kila jambo utapata matokeo makubwa katika maisha yako
No comments:
Post a Comment